MANDONGA AREJEA NA NGUMI YA KIBERENGE MULEBA

BONDIA wa ngumi za kulipwa, Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’ amemtangazia vita mpinzani wake ajipange kuelekea pambano katika pambano la ‘Tagi la Mama Samia’ litakalofanyika Desemba 26 mjini Muleba mkoani Kagera.

Dullah Mbabe atapanda ulingoni kuzichapa pambano kuu (Main Card) dhidi ya Maugo litakalochezwa raundi nane, uzito wa juu ( kilo 76) litakalofanyika Muleba Mkoani Kagera.

Akizungumza Dar es Salaam katika uzinduzi wa pambano hilo, Dullah Mbabe alisema baada ya kukaa kimya muda mrefu bila kupanda ulingoni awamu hii amejipanga kuja kuleta mapinduzi katika ngumi.

Ă€lisema kuwa amemwambia mpinzani wake ajiandae na anemwomba promota kuandaa gari la qagonjwa kwa ajli ya mpinzani wake.

“Niko salama kiafya naendelea vizuri, naenda katika vita yule Mada Maugo, baada ya kupoteza mapambano machache ikiwemo la Erick Katompa naenda kuonyesha kazi mkoani Kagera.

“Watanzania na wakazi wa Muleba wategemee mambo mazuri kutoka kwangu, kwani siku hiyo nitamuonyesha kazi kwa sababu mara ya kwanza nilimteuwa kiuno awamu hii zamu yake “alisema Dullah Mbabe.

Naye Mratibu wa matukio kutoka Kampuni ya Peak Time, Bakari Khatibu ambao ndiyo waandaji wa pambano hilo alisema awamu hii wanaenda kuweka historia Muleba kutokana na mapambano hayo.

“Awamu hii kuna mapambano makali ambayo watanzania na Muleba watashuhudia kwa sababu mabondia wakali watapanda ulingoni kuonyesha kazi, “alisema Khatibu.

Kwa upande wa bondia, Karim Mandonga alisema mpinzani wake, Said Mbelwa amalizi raundi ya pili kutokana na maandalizi anayoyafanya.

Alisema anaenda mkoani Kagera kuonyesha ngumi mpya itwayo ‘Kiberege’ ambayo itaenda kumpiga mpinzani wake, Mbelwa.

Mbali ya mabondia hao mapambano mengine ambayo siku hiyo yataenda kuonyesha kazi ni pamoja na Osama Arabi atacheza na Peter wakati Anuari Mlawa dhidi ya Rashidi Matumla huku Jamali Kunoga atazichapa na Khalidi Kunoga wakati Happy Daudi dhidi ya Hidaya Zahoro.

Related Posts