Majeruhi TZ Prisons wamliza Makatta

KOCHA wa Tanzania Prisons, Mbwana Makatta aliyeishuhudia timu hiyo ikimaliza ikiwa pungufu uwanjani mbele ya Kagera Sugar ikitoka suluhu kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba amesema idadi ya majeruhi imechangania kuwa na mwendeno mbovu Ligi Kuu.

Prisons iliyopo nafasi ya 12 ikiwa na pointi 11 kupitia mechi 13 ikishinda miwili, sare tano na kupoteza sita sawa na idadi ya mabao ya kufungwa na kufungwa 11, imemfanya Makata kukiri hali si nzuri.

Kocha huyo ameliambia Mwanaspoti kuwa idadi kubwa ya majeruhi imechangia kupata matokeo yasiyoridhisha katika mechi walizocheza hadi sasa.

Aliwataja walioumia kuwa ni washambuliaji Samson Mbangula, Jeremiah Mgunda na mabeki Nurdin Chona na Benedicto Jacob ambao wametia doa kikosi hicho, licha ya waliosalia kupambana sana, lakini matokeo hayapo upande wao.

“Unajua kukosa wachezaji muhimu kama hao lazima upungufu utokee kwenye timu,” alisema.

Kocha huyo wa zamani wa Dodoma Jiji aliongeza kuwa nyota wapya aliowapa nafasi ya kuziba pengo la majeruhi wanaonyesha kuwa washindani hivyo anaamini watakuwa bora zaidi siku za usoni.

Related Posts