Idris azidi kung’ara Netflix – Millard Ayo

Mchekeshaji Mwigizaji super star, Idris Sultan ameipa heshima tasnia ya Filamu Tanzania akiwa nchini Afrika Kusini ambako alikua kwenye mualiko maalumu kutoka Platform ya Netflix kwa ajili ya msimu mpya wa tamthiliya ya Bridgerton ambayo ameshiriki ndani yake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Idriss Sultan alipost baadhi ya picha na video akiwa na mastaa mbalimabli walioalikwa na Netflix akiwemo Elsa Majimbo kutoka Kenya. Post hizo zikiwa na maandishi yenye maswali ya kujua ‘What’s next from Idris Sultan?’, kwenye moja ya post yake aliandika “Prince from the East” ndo nimepewa hiyo…

Akiwa Afrika kusini Idris Sultan alikua miongoni mwa wasanii walipendeza sana, kiasi cha kuvutia mastaa mbalimbali waliokua kwenye onesho hilo lililopewa jina la ‘Regency Era Splendor: Into The Spotlight’ lililofanyika Mei 4, mwaka huu nchini Afrika Kusini, ambapo Netflix, waandaaji wa series hiyo, walizindua msimu wa tatu wa Bridgerton, katika jiji la Johannesburg, na kuhudhuliwa na mastaa mbalimbali wa filamu barani Afrika, kama vile Nigeria, Kenya, Ghana, Zimbabwe, Botswana na Afrika Kusini.

Msimu wa kwanza wa tamthilia Bridgerton ilianza kuruka December 25, 2020, Msimu huu mpya wa tatu wa Bridgerton unatarajiwa kurushwa na Netflix na kushuhudiwa na ulimwengu mzima Mei 16, mwaka huu ambapo itaruka sehemu ya kwanza na sehemu ya pili Juni 13, mwaka huu.

Related Posts