SERIKALI KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU KUFANYA MAPITIO YA MABORESHO KANUNI NA SHERIA SEKTA YA UVUVI


Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na wadau wa sekta ya Uvuvi imekutana na kufanya kikao kazi cha mapitio ya kanuni na sheria za Sekta hiyo kwa lengo la kufanya maboresho  kulingana na mabadiliko ya Tabia ya nchi.


Akifungua kikao hicho kilichofanyila leo tarehe Desemba 6, 2024 katika ukumbi ulipo Uvuvi House jijini Dar Es Salaam Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Edwin Mhede amesema kikao hicho kimeandaliwa  kwajili ya kusikiliza maoni ya wadau wa sekta ya uvuvi.


“Uzoefu wenu na maarifa yenu ni muhimu sana katika kutengeneza kanuni zitakazo tumika kama Mwongozo muhimu wa usimamizi wa Sekta ya Uvuvi” amesema Dkt Mhede 


Aidha Dkt Mhede ameongeza kuwa ili kuwa na usimamizi madhubuti katika sekta hiyo ni lazima kuwe na mfumo mzuri wa kanuni na sheria zitakazo zingatia na kulinda maslahi ya wawekezeji pamoja na rasilimali za nchi yetu.


Vilevile Dkt. Mhede amewasihi wadau walioshiriki katika kikao hicho kutoa maoni pamoja na napendekezo yao kwa uhuru ili kusaidia kuboresha kanuni na sheria za sekta hiyo.


Naye Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Neema Mwanda amesema kuwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeamua kufanya mapitio ya kanuni na sheria za sekta hiyo ili ziweze kuendana na mahitaji ya sasa ikiwemo kutatua changamoto zilizopo pamoja na kuendeleza Tasnia ya Uvuvi kwa ijumla.

Related Posts