Baadhi ya askari Mkoa wa Kipolisi Ilala, wakiwa katika maandamano ya amani yaliolenga kuunga mkono juhudi za Serikali na jamii kupinga ukatili wa kijinsia. |
Maandamano ya amani ya askari na wanafunzi wa shule za msingi yakilenga kuunga mkono juhudi za Serikali na jamii kupinga ukatili wa kijinsia. |
Baadhi ya askari Mkoa wa Kipolisi Ilala, wananchi na wanafunzi wa shule za msingi wakiwa katika maandamano ya amani yaliolenga kuunga mkono juhudi za Serikali na jamii kupinga ukatili wa kijinsia. |
Baadhi ya askari Mkoa wa Kipolisi Ilala, na wanafunzi wa shule za msingi wakiwa katika maandamano ya amani yaliolenga kuunga mkono juhudi za Serikali na jamii kupinga ukatili wa kijinsia. |

JESHI la Polisi katika Mkoa wa Kipolisi wa Ilala (Dar es Salaam) limetoa mwito kwa wanaume wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia na wake zao hususan kupigwa na mwingine wowote kujitokeza na kutoa taarifa katika vituo vya polisi ili hatua stahi zichukuliwe dhidi ya wahusika.
Aidha, Ofisa Elimu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, (Msingi na Awali), Mwalimu Margareti Macha amesema ukatili huathiri watoto kwa namna mbalimbali zikiwamo za kimwili, kisaikolojia na kimasomo hivyo, kuharibu maisha ya Watoto wengi.
Hayo yamebainishwa katika maandanano ya polisi katika Mkoa wa Kipolisi wa Dar es Salaam na wanafunzi wa shule za msingi katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam yaliiongozwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Yustino Mgonja jana kutoka Tabata Shue mbele ya Kitu cha Polisi hadi Baracuda kama sehemu ya maadhimisho ya Kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia.
Kwa mujibu ofisa elimu huyo, takwimu za Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) za mwaka 2009 zinabainisha kuwa wastani wa mtoto mmoja kati ya watoto saba wa kuime huathiriwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia ukiwamo wa kingono.
Amesema: “Wazazi tuwe makini hasa katika suala la watoto kulala na wageni maana wakati mwingine hata baadhi ya wajomba na mashangazi wanahusika na ukatili wa kijinsia kwa watoto,” amesema Macha.
Kamanda Mgonja na Mkuu wa Mtandao wa Polisi Wanawake katika Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Hassina Ramadhani Taufiq wamesema elimu sahihi kwa jamii na hususan watoto na vijana inahitaji zaidi ili kukabili tatizo na kwamba, ndio maana Jeshi la Polisi limelivalia njuga.
Mgonja amesema: “Watoto na wanawake ni waathirika wakubwa, lakini hata wanaume wapo wanaonyanyaswa hivyo, wajitokeze kwenye vyombo husika ili kupata maada na ufumbuzi… ingawa hawasemi, ukatili huu unawaathiri baadhi ya wanaume hivyo, lazima kuwepo nguvu za amoja kuutokomeza.”
Naye Mkuu wa Mtandao wa Polisi Wanawake ambaye ni Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Taufiq amesema: “Ukatili wa kijinsia haubagui jinsia, bali wote wanawake, wanaume na watoto hivyo, hata wanaume wanaofanyiwa ukatili ukiwamo wa kupigwa, waje polisi tuwasaidie kupata ufumbuzi.”