Bodi ya TASAC :Kukamilika kwa Bandari ya Mbamba Bay kufungua maendeleo ya Kiuchumi

*Watoa shukrani kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kutoa fedha ujenzi wa Bandari ya Mbamba Bay.

Na Mwandishi Wetu,Nyasa

Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Meli Tanzania (TASAC) limesema kuwa Bandari ya Mbamba Bay katika Ziwa Nyasa mkoani Ruvuma ni Muhinu katika Maendeleo ya Kiuchumi.

Bandari hiyo itafungua biashara katika nchi za Malawi ,Zambia pamoja na Msumbiji katika usafirishaji wa mizigo ya makaa ya mawe pamoja na mazao katika mikoa inayoizunguka ziwa hilo.

Akizungumza katika ziara ya Bodi hiyo katika Bandari ya Mbamba Bay Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC Nah.Mussa Mandia amesema kuwa serikali imewekeza zaidi ya sh.bilioni 80 ambapo ujenzi wa Bandari hiyo unatarajiwa kukamilika 2026.

Amesema kuwa fedha hizo zimetolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutambua umuhimu wa kujengwa kwa bandari ya kisasa katika Bandari ya Mbamba Bay.

Amesema kuwa bandari hiyo itakuwa na huduma zote ikiwa TASAC wadhibiti na wasimamizi vyombo vya Usafiri majini kuhakikisha usalama unazingatiwa.

Nah.Mandia amesema bandari hiyo zamani ilikuwa changamoto ya Barabara lakini suala hilo serikali ilishakamilisha kwa asilimia 100.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Nelson Mlali amesema hatua nzuri kwa ujenzi wa bandari kutokana na kuwepo miundombinu barabara hadi bandarini.

Amesema kuwa bandari hiyo ipo katika eneo sahihi katika kuchochea fursa za kiuchumi kwa wakazi wa Nyasa pamoja nchi jirani kutumia katika kusafirisha mizigo kwa kutumia bandari hiyo.

Mhandisi Mkuu Bandari za Ziwa Nyasa Fabian Paul anaeleza hatua zilizofikiwa kwenye mradi huo wa mikakati kwa nchi.

Amesema kuwa ujenzi huo umefikia zaidi ya asilimia tisa na kufikia hapo kulitokana kuchelewa kwa vifaa.

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Peres Magiri amesema bandari hiyo inafungua milango kwa wawekezaji wa sekta mbalimbali huku wananchi wa Wilaya ya Nyasa wakiamini kuwa kukamilika kwa bandari hiyo kwao ni fursa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Nah.Mussa Mandia akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Peres Magiri wakati Bodi  hiyo ilipotembelea Ofisi hiyo kwa ajili ya ziara ya Bandari ya Mbamba Bay iliyopo Ziwa Nyasa mkoani Ruvuma.
 

Mhandisi  wa Ujenzi wa Bandari ya Mbamba Bay Rafiki Joseph akitoa maelezo  kwa Bodi ya Wakurugenzi wa TASAC wakati ilipotembelea Bandari hiyo.
 

Mhandisi Mkuu Bandari za Ziwa Nyasa wa TPA  Fabian Paul akitoa maelezo  kwa Bodi ya Wakurugenzi wa TASAC wakati ilipotembelea Bandari hiyo.
 

Picha ya pamoja ya Bodi ya Wakurugenzi  wa Shirika la Uwakala wa Meli  (TASAC) wakiwa na Watendaji wa TASAC pamoja na Watendaji wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA ) katika Bandari ya Mbamba Bay

Related Posts