OFISA Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB), Almas Kasongo amevunja ukimya na kutoa ufafanuzi juu ya nafasi ya mwenyekiti wa bodi hiyo, Steven Mguto ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Coastal Union.
Mguto kwa sasa sio miongoni mwa wagombea 17 waliojitokeza kuwania nafasi katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo ya Coastal kwa vikle hakugombea kabisa.
Kassongo ametoa ufafanuzi huo alipozungumza na Mwanaspoti lililotaka kujua juu ya mwenyekiti wa sasa wa Bodi anatakiwa awe ni kiongozi wa klabu yeyote, hivyo kwa hali ilivyo kwa Mnguto mara baada ya uchaguzi wa klabu ya Coastal atapoteza sifa wa kuendelea kuwa mwenyekiti wa bodi hiyo.
Kasongo amesema Mnguto ataendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo hadi katika mkutano mkuu wa 12 wa bodi hiyo ambao utafanyika Desemba mwakani.
“Uchaguzi Mkuu wa Coastal utafanyika baada ya mkutano mkuu, hivyo mwenyekiti aliyepo sasa ataendelea kutambulika kama Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi hadi pale mkutano mkuu wa bodi hiyo utakapofanyika ambapo utafanyika uchaguzi wa kumchagua mwenyekiti mwingine,” amesema Kasongo.
Mnguto alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB), Desemba Mosi, mwaka 2018 katika uchaguzi mkuu uliofanyika jijini Tanga, alipowania akiwa pekee yake na kupigiwa kura za ndio 16 kati ya 18, huku wajumbe wa Yanga na African Lyon hawakushiriki uchaguzi huo.
Leo Jumamosi Bodi ya Ligi Kuu itafanya mkutano mkuu kwenye hoteli ya Lake Tanganyika, iliyopo mjini Kigoma huku mkutano huo ukitarajiwa kuhudhuriwa na watu zaidi ya 200.
Juu ya mkutano huo, Kasongo amesema mkutano huo utakuwa na agenda zisizopungua 11 ambapo uchaguzi mdogo kujaza nafasi za wajumbe wawili utafanyika