Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC)Nahodha Mussa Mandia akizungumza na wananchi na wavuvi katika Mwalo wa Njambe katika Ziwa Nyasa wakati ziara ya kutembelea ziwa hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC)Nahodha Mussa Mandia akisalimiana na kijana ambaye ni fundi boti ndogo katika Mwalo wa Njambe katika Ziwa Nyasa wakati ziara ya kutembelea ziwa hilo.
Na Mwandishi Wetu,Nyasa
BODI ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli (TASAC) imesema kuwa kazi ya udhibiti kwao ni pamoja na kuangalia usalama wa vyombo vidogo vya majini pamoja usafirishaji abiria
Hayo ameseyasema Mwenyekiti wa Bodi hiyo Nahodha Mussa Mandia wakati bodi hiyo ilipotembelea mwalo wa Njambe katika Ziwa Nyasa wilayani Nyasa mkoani Ruvuma.
Amesema kuwa wavuvi katika mwalo huo ni lazima kuzingatia usalama pamoja na kuwa na vifaa vya uokozi.
Aidha amesema kuwa vyombo vya uvuvi lazima viwevimesajiliwa pamoja na kuwa vifaa vya uokozi huku akiwataka waendeshaji wa vyombo hivyo kukataa ikiwa njia ya kuwafanya wamiliki kuwa na vifaa vya uokozi.
Hata hivyo amesema kuwa mazingira ya eneo wanafanyia kazi kwa kuwa mazingira usafi ni pamoja na kuwa huduma za choo.
Hata hivyo amesema ziara hiyo ni pamoja kuwatembelea wananchi kuwasiliza masuala ambayo ni changamoto ili kufanyia kazi.
Amesema kuwa serikali ya Dkt.Samia Suluhu Hassan imekuwa ni serikali ya kufanya kazi kwa vitendo.