Dodoma Jiji nje Shirikisho, Leo Tena yatakata

TIMU za Ligi Kuu zinaendelea kupungua kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya Dodoma Jiji nayo kuaga kufuatia kipigo cha penalti 5-6 dhidi ya Leo Tena ya mkoani Kagera.

Leo Tena inayoshiriki Ligi Daraja la Tatu Mkoa wa Kagera, inaungana na Mambali Ushirikiano ya mkoani Tabora iliyoiaibisha mapema Ken Gold kwa penalti 3-4 baada ya sare ya 1-1 katika dakika 90.

Licha ya timu za Ligi Kuu kupewa nafasi ya kuanzia nyumbani, lakini Ken Gold na Dodoma Jiji zimejikuta zikisukumwa nje kufuatia matokeo hayo.

Katika mchezo huo  ambao umepigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, ilishuhudiwa dakika 90 zikiisha kwa sare ya bao 1-1 baada ya wenyeji kutangulia kabla ya wageni kusawazisha kisha kutakata  kwenye penalti.

Matokeo mengine, Azam imeichakaza Iringa SC mabao 4-0, KMC ikiizaba 5-0 Black Six, Pamba Jiji ikiilima bao 1-0 Moro Kids, Coastal Union ikiilaza Stand FC 4-0 na Fountain Gate ikiizima 2-0 Mweta SC ya Mwanza.

Related Posts