Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) imetumia Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani(ICAD) kushiriki katika mbio za Marathon zilizoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Mbio hizo zilizoongozwa na Mhe Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko akiwa na Mkuu wa Chuo Kikuu Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete ambaye ni mbunge wa Mchinga pamoja na uongozi wote wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani (ICAD) ambayo kilele chake ni Desemba 7,2024. Maadhimisho ya mwaka huu pia inatimia miaka 80 tangu siku hii ilipoanza kuadhimishwa mnamo Desemba 7 mwaka 1944.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameongoza mbio za UDSM Marathon za Chuo Kikuu cha Dar es salaam akiwa na Mkuu wa Chuo Kikuu Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete ambaye ni mbunge wa Mchinga pamoja na uongozi wote wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) pamoja na wadau mbalimbali wakiwa kwenye Matembezi na Mbio zilijulikanazo kama UDSM Marathon
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA wakiwa kwenye picha ya pamoja