UKANDA WA KUSINI WAJIPANGA KUBORESHA MIFUMO YA MAJI SAFI NA MAZINGIRA

Wadau wanaotekeleza miradi mbalimbali ya maji Mkoani Lindi wamekutana kwa pamoja kujadili namna ya bora ya kuendelea kuboresha mifumo ya maji safi na usafi wa mazingira kwa ukanda wa kusini.

Mkutano huo umefanyika Mjini Lindi kwa siku mbili kuanzia Disemba 5 hadi 6,2024 ukikutanisha Serikali na wadau kutoka katika mashirika na taasisi mbalimbali ikiwemo Heart foundation chini ya ufadhili wa Koica,Kanisa la Anglican Dayosisi ya Masasi wakishirikiana na World Vision na wawakilishi kutoka katika jamii ambayo wadau hao wamekuwa wakitekeleza miradi ya maji pamoja na ujenzi wa vyoo bora kama halmashauri ya Mtama.

Mratibu wa Mirradi kutoka shirika la Heart to Heart Foundation Innocent Deus ameeleza kwa upande wa Mkoa wa Lindi hapakuwahi kuwa na jukwaa la kuwakutanisha wadau hao pamoja kujadili mafanikio na nafasi zao za uwekezaji kwenye miradi ya maji hivyo kwa mwaka huu wameona ni vyema kukutana ili pia waweze kuainisha maeneo ambayo bado yanachangamoto jambo litakalosaidia pia kuvuta wadau wengine waweze kuyafanyia kazi.

Amesema maeneo mengi ambayo wadau wanatekeleza miradi ya maji ikiwemo halmshauri ya Mtama ambako wao wamejikita kujenga miradi ya maji na ujenzi wa vyoo kwenye maeneo ya shule na vituo vya kutolea huduma za afya hali imebadilika ukilinganisha na huko nyuma ambako ujenzi wa vyoo ulikuwa chini na upatikanaji wa maji safi hali ambayo imerahisisha huduma kwa kwenye maeneo husika.

Akieleza namna wanavyoshirikiana na serikali kutatua changamoto za maji Mkoani Lindi kupitia wakala wa maji ya usafi wa mazingira Vijijini Ruwasa George Mgaza kutoka Kanisa la Anglikan Dayosisi ya Masasi amesema wamekuwa wakishiriki kujenga na kufanya kampeni mbalimbali za maji katika maeneo ya vijiji vya Mipingo na Lihimilo (Mchinga)na Mtama katika maeneo ya Namupa,Mahiwa na Mandwanga.

Amebanisha kuwa yote hayo ni katika kuhakikisha jamii si tu inapata maji bali hata inaboresha mazingira yake kwa kujenga vyoo bora na kuvitumia kwa lengo la kupunguza changamoto zinazotokana na athari za uchafuzi wa mazingira hususan magonjwa kama vile kipindupindu.

Kwa upande Mkuu wa Wilaya ya Lindi Victoria Mwanziva ambaye alipata nafasi ya kusikiliza mawasilisho mbalimbali kutoka kwa wadau hao na baadae kufunga mkutano huo amewapongeza Heart to Heart kwa kuandaa mkutano huo ambao anataswira yakuboresha miradi ya maji na usafi wa mazingira kwenye wilaya hiyo akiahidi kama serikali watahakikisha wanawaunga mkono na kuisimamia miradi yao ili ilete tija kwa jamii.

Aidha,amewaomba wadau hao kuendelea kuwa wabunifu na kuibeba agenda ya WASH ili iwe yakudumu katika maeneo yao sambamba nakuwapa elimu wawakilishi wa wananchi kama madiwani na wenyeviti wa vijiji,vitongoji na mitaa wapya waweze kuisimamia vizuri miradi na kusaidia kuhamasisha jamii katika ujenzi wa vyoo bora na kuvitumia.

 

Related Posts