TASAC yakazia uboreshaji huduma za abiria Liuli,Njambe na Manda

Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) imeelekeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kujenga jengo la abiria vyoo pamoja kuweka mnara wa taa utakaosaidia kuongoza vyombo vya usafiri majini nyakati za usiku katika ziwa Nyasa.

Akizungumza na wananchi katika bandari ya Liuli,Njambe na Manda, tarehe 05 Dedemba, 2024, wakati wa ziara ya bodi ya TASAC, Mwenyekiti wa Bodi, Nah. Mussa Mandia amesema bandari hizo zinawahudumia wananchi wengi wanaoishi pembezoni mwa ukanda wa ziwa Nyasa na wanaposhuka au wakati wakisubiri kupanda meli hiyo hukosa mahali pa kujisitiri na mvua,jua na kukosa huduma stahiki za vyoo.

“Wananchi wengi wanapata huduma za usafiri kupitia bandari hizi tumejionea bandari ya Liuli,Njambe na Manda zina changamoto zinazofanana ambazo zinagusa taasisi mbalimbali.Sisi tumezichukuwa na tutawajulisha taasisi zinazohusika ili ziweze kufanyiwa kazi.

Suala la jengo la kupumzika abiria na hufuma ya vyoo hili ni la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na wamishaweka mipango ya utatuzi ndani ya mwaka huu wa fedha.

Nawaelekeza wafanye haraka watekeleze ujenzi wa miundo mbinu hiyo bila kuchelewa”. Amesema Bw.Mandia.

Naye mhandisi Fabian Paulo amesema kuwa mipango imishafanyika na bajeti imepengwa ya kujenga majengo ya abiria, vyoo na uwekaji minara ya taa zinazotumia nguvu ya jua ili kuwezesha bandari hizo kutoa huduma bora na salama.

Tunao mpango mkakati wa namna ya kuboresha huduma za usafiri kwa wananchi wanaotegemea ziwa Nyasa katika kusafiri na kujipatia kipato.Taa za nguvu ya jua zimishanunuliwa na fedha imetengwa ndani ya mwaka huu wa fedha 2024/25 tutajenga majengo ya abiria, vyoo na minara katika bandari ya Liuli,Lundo,Njambe na Manda.Tunaomba Serikali ya kijiji husika kutenga maeneo ya ujenzi wa majengo na vyoo hivyo ili tutakapokuja tupate tayari eneo limetengwa.Kama unavyoona maeneo haya wananchi wamejengwa karibu na ziwa”.Amesema Bw.Paul.

Wananchi walipaza sauti zao kuomba huduma za vyoo,mnara wa kuongezea boti za uvuvi nyakati za usiku pamoja na jengo la abiria kupata kivuli na kujinga mvua.

“Naomba Serikali itujengee huduma ya choo kwa sababu abiria wanapokuwa wanaotoka na wanaopanda kwenye meli hawana sehemu ya kujisaidia”. Amesema Bwana George Patriki.

Naye Bwana Edward Mpangala amesema usalama wao ni mdogo kwa sababu ziwa halina taa za kuwaongoza wasipotee uelekeo pale wanakuwa kwenye eneo la mbali na nchi kavu.

“Usalama kuendesha boti za uvuvi kwa sasa hakuna kwa sababu hakuna mnara wa taa unaonyesha maeneo ya bandari tunazotoka”.Amesema Bw.Mpangala

Bodi imeielekeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kuzingatia usalama na taasisi zingine kusogeza huduma za kijamii ikiwemo umeme na barabara ili kuzifanya bandari hizo zitoe huduma bora kwa wananchi.

 

Related Posts