CPA MALUNDO,WENZAKE WANNE WATUNUKIWA UDAKTARI WA HESHIMA NA CHUO CHA MAREKANI

Na Mwandishi wetu

MKURUGENZI wa Kampuni ya Y.h.Malundo & Co inayojishughulisha na Uhasibu,Ukaguzi wa Hesabu,Ushauri wa Kodi na Menejimenti ya Fedha, CPA.Yona Malundo ametunukiwa shahada ya Udaktari wa heshima na Chuo Kikuu cha Lead Impact cha nchini Marekani kutokana na kutambua mchango wake kwenye jamii pamoja na uendeshaji wa shughuli zake kwa usahihi,kuzingatia maadili na ufanisi mkubwa.

Akitunukiwa shahada hiyo wakati wa mahafali ya nane tangu Chuo hicho kianze kuwatunukia watanzania nchini,Dkt.CPA. Malundo alisema udaktari aliotunukiwa atautumia kwa kuendelea kuwasaidia watu wasiojiweza kwasababu ndio kitu anachokifanya kwa jamii.

Alisema tangu alipofungua kampuni yake imekuwa ikifanya kazi na watu mbalimbali bila kubagua wenye vipato vikubwa wala kidogo katika kuwafanyia kazi zao.

”Nakishukuru Chuo hiki kwa kutambua juhudi zangu katika jamii kwa muda wa miaka kumi,kupitia kampuni yangu nimekuwa nikifanya kazi na watu wenye vipato tofauti tofauti vya chini na juu na pia kuwa mstari wa mbele katika kusaidia jamii,”alisema.

Alisema kupitia shahada hiyo ya udaktari atahakikisha anaendelea kuitumikia jamii ipasavyo na kuwasaidi kwa namna moja au nyingi ilikuona kuwa watanzania wote kuwa sawa.

Awali akizungumza katika hafla hiyo Mratibu Mkuu wa Chuo hicho nchini, Askofu Dkt. Peter Rashid Abubakar alisema chuo hicho maarufu ulimwenguni kinatunukia Udaktari wa Heshima kwa watu wa kada mbalimbali kulingana na sifa na mchango anaoutoa katika jamii.

“Hiki chuo ni maarufu sana na kiko nchini Marekani, kinatunuku Udaktari wa Heshima kuendana na CV ya mtu na mchango wake kwa jamii na taifa kwa ujumla. Tayari tumeshatoa shahada za Udaktari wa Heshima kwa viongozi mbalimbali hapa nchini,” alisema.

Aliongeza kuwa chuo hicho kimekuwa kikitoa shahada hiyo kwa wanasiasa, wafanyabiashara na viongozi wa dini na kina mpango wa kuanzisha tawi lake hapa nchini.

Aidha Dkt. Rashid ambaye ndiye Mratibu wa Chuo hicho kwa nchi tano ikiwemo Tanzania, Rwanda, Uganda na nyinginezo, aliwapongeza waliotunukiwa udaktari huo na kusema kuwa wamefanya kazi zao nzuri za kusaidia jamii.

”Chuo hicho msingi wake ni dini na Shahada hii ya udaktari wa heshima tuliyotoa kwa Watunukiwa hao ni kutokana na kazi nzuri zilizoonekana baada ya kuwafilia kwa kipindi cha muda mrefu hadi kuwatunuku.

Akitaja watunukiwa wengine waliopata udaktari wa heshima ni pamoja na Mkurugenzi Mkuu Jenga Africa Empowering Society Build Nation (ESBN),Dkt Paul Kanijo,Mkurugenzi wa Mesodate Consultants ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Millenium Solution Development Trust Fund, Dkt Emmanuel Jeremiah.

Wengine ni Dk Boniface Mbelwa na mkewe Dk Chriatian Robert Mbelwa ambao ni mke na mume.

Naye Diwani wa Viti Maalum wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Dk Juliet Banigwa aliwapongeza madaktari wenzake kwa tuzo hizo za udaktari sambamba na kumshukuru Dk Rashid ambaye ni msimamizi wa chuo hicho tawi la Tanzania.

Dkt Juliet alisema shahada hizo za udaktari ni furaha na heshima kubwa kwa nchi kwani wataendelea kuwainua na kuwaimarisha watu na jamii kwa ujumla.

Related Posts