UJENZI WA MAJENGO MAPYA IMS ZANZIBAR WAFIKIA ASILIMIA 50

NA EMMANUEL MBATILO, ZANZIBAR

UJENZI wa majengo ya mabweni na jengo la utawala katika Taasisi ya Sayansi za Baharini (IMS) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), iliyopo Buyu visiwani Zanzibar umefikia asilimia 50 kukamilika.

Ukiwa unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Agosti 2025 na kuanza kutumika, ujenzi huo ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) ambao ni sehemu fedha za mkopo kutoka Benki ya Dunia kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Akizungumza mara baada ya kutembelea mradi huo December 8,, 2024 visiwani hapo, Mkuu wa UDSM, Rais Mtaafu Dkt Jakaya Kikwete ameelezea kuridhishwa kwake na kasi ya ujenzi huo ilio chini ya Chuo Kikuu hicho, na kuthibitisha kwamba ifikapo Agosti 2025, mradi utakuwa umekamilika.

Aidha Dkt. Kikwete amesema dhumuni la ujenzi wa taasisi hiyo ni kuwa Kituo kikubwa cha utafiti katika masuala yanayohusu sayansi ya bahari ambacho kitakuwa cha kipekee katika ukanda huo.

“Tutakapokuwa tumekamilisha mradi huu, maabara ambazo zitakuwepo, wahadhiri watakaopatikana, tutakifikisha kwenye kiwango hicho na hapo ndipo tutakapokijenga chuo chetu kama ni kituo muhimu katika tafiti za bahari na viumbe bahari “. Amesema

Kwa upande wake Naibu Mratibu wa Mradi wa HEET, UDSM, Dkt. Liberato Haule amesema mradi huo ambao ni wa thamani ya shilingi bilioni 11.1 ulionza kutekelezwa baada kusaini mkataba na mkandarasi mwezi wa pili mwaka huu, utakabidhiwa baada ya miezi 18, ambapo ni Agosti mwakani, na kueleza kuwa tayari mkandarasi amekwisha lipwa kiasi cha shilingi bilioni 3.6 kama sehemu ya mkataba.

Amesema jenzi utakapokamilika utaleta mabadiliko makubwa ambapo kwasasa taasisi hiyo inauwezo wa kuchukua wanafunzi takribani 139 na wanatarajia ujenzi ukikamilika watakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 280.

“Vyumba vyote vya maabara vitakuwa na vifaa ambavyo vipo kwenye bajeti ya mradi wa HEET kwahiyo punde ujenzi utakapokamilika, tutakuwa tumefunga hivyo vifaa ambavyo sasa hivi tupo kwenye hatua za awali za kuanza ununuzi wa vifaa hivyo”. Amesema

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akizungumza na waandishi wa habari wakati akiwa kwenye ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi katika Taasisi ya Sayansi za Bahari, kampasi ya Buyu, iliyopo takribani kilomita 13 kusini mwa Mji Mkongwe wa Zanzibar.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa kwenye ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi katika Taasisi ya Sayansi za Bahari, kampasi ya Buyu, iliyopo takribani kilomita 13 kusini mwa Mji Mkongwe wa Zanzibar.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa kwenye ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi katika Taasisi ya Sayansi za Bahari, kampasi ya Buyu, iliyopo takribani kilomita 13 kusini mwa Mji Mkongwe wa Zanzibar.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akipata picha ya kumbukumbu na uongozi wa chuo na wakandarasi baada ya kuhitimisha ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi katika Taasisi ya Sayansi za Bahari, kampasi ya Buyu, iliyopo takribani kilomita 13 kusini mwa Mji Mkongwe wa Zanzibar.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akionesha kampasi itakavyokuwa wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi katika Taasisi ya Sayansi za Bahari, kampasi ya Buyu, iliyopo takribani kilomita 13 kusini mwa Mji Mkongwe wa Zanzibar.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO PAMOJA NA ISSA MICHUZI)

Related Posts