Meya wa Jiji la Arusha Aibuka na Miradi ya Maendeleo jiji la Arusha.

 

Na Jane Edward, Arusha 

Wananchi Jijini Arusha wametakiwa kuwa na uzalendo kwa kuendelea kuwa na imani na serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha Maximillian Iraghe amesema Serikali kupitia halmashauri ya jiji la Arusha inaendelea kukamilisha miradi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara, vyumba vya madarasa,pamoja na uboreshaji wa vituo vya afya.
Amesema kupitia baraza la madiwani lililofanyika Novemba sita limeazimia manunuzi ya greda kwaajili ya kukamilisha miradi ya barabara.
 Aidha amesema kuwa, baraza limeelekeza utoaji wa vibali vya ujenzi unaozingatia sheria pamoja na maendeleo ya mji, sehemu ya jiji ambayo ina mitaa ya biashara na majengo makuu ya umma ikijumuishwa na viwanda, makazi, biashara.
Ameongeza  kuwa, baraza pia limeelekeza uitishwe mkutano wa dharura wa baraza la madiwani kwa kuwashirikisha TARURA ,TANROADs na AUWSA ili kujadili kwa kina changamoto ya barabara kwenye mitaa ya jiji la Arusha na kuweza kutatuliwa kwa wakati ili wananchi waweze kuondokana na changamoto hiyo.

 

Related Posts