AFRIKA TUKUZE UCHUMI WA VYAMA VYAMA VYETU

Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Chama Cha Mapinduzi Zanzibar Dkt. Mohammed Said Mohammed (katikati) akikabidhi cheti kwa mshiriki wa mafunzo hayo wakwanza kulia ni Mkuu wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Prof Marcellina Chijoriga.

Na Khadija Kalili, Michuzi Tv

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dkt. Mohammed Said Mohammed amesema wakati umefika kwa nchi na vyama rafuki zilizo Kusini mwa Afrika kukuza uchumi wa vyama vyao.

Dkt. Mohammed amesema hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya kufunga mafunzo ya siku saba ya makada kutoka vyama sita rafiki vilivyoko Kusini mwa Afrika yaliyohitimishwa tarehe 8 Desemba ,2024 ambayo yamefanyika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Kwamfipa Kibaha Mkoani Pwani.

Mafunzo hayo ambayo yamefanyika kati ya tarehe 2 Desemba na kufungwa jana tarehe 8 Desemba , 2024 ambayo ni mafunzo ya 13 ya Uongozi ya mapitio ya juhudi za kuleta mabadiliko ya kisasa katika nyanja za maendeleo yaliyohusisha vijana viongozi kutoka nchi sita za kusini mwa Afrika katika harakati za maendeleo yaliyofadhiliwa na Chama Cha Kikomunisti cha nchini China (CPC).

Aidha Dkt Mohammed amesema kuwa anatoa pongezi nyingi kwa Chama Cha CPC ambacho kutokana urafiki wao wa muda mrefu mrefu wamekua wakitoa msaada kwa vyama sita rafiki kabla na baada ya ukombozi Kusini mwa Afrika ambapo hivi sasa wamegeukia kwenye kusaidia bara la Afrika katika sekta za afya, usafiri,kukuza uchumi na kujenga viwanda mbalimbali ambavyo pia vimekua vikitoa ajira.

Akizungumzia kuhusu mafunzo hayo amesema kuwa ni nguzo muhimu ya kukuza ushirikiano baina ya nchi na vyama rafiki sita ikiwamo CPC.

“Wakati umefika kuwa tunatakiwa kuwekeza katika uchumi hasa kwa vizazi vyetu tunavyojadili maendeleo ya siasa yaende sambamba na kutafuta mbinu za kukuza uchumi wa vyama vyetu kwa ujumla” amesema Dkt.Mohammed.

“Tunahistoria ya mshikamano wa kweli nina imani kubwa ushirikiano huu uendelee katika kukuza uchumi wa nchi zetu kiuchumi kwakuwa China wamekua wakiisaidia Afrika “amesema Dkt Mohammed.

Mkuu wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Prof Marcellina Chijoriga amewasisitiza wahitimu hao kupambana na vitendo vya rushwa ndani ya vyama vyao kwa sababu vitendo hivyo huleta mgawanyiko miongoni mwao.

Mafunzo hayo yameshirikisha washiriki 120 ambao wametoka kwenye vyama rafiki Kusini mwa Afrika ambavyo ni ANC (Afrika ya Kusini), FRELIMO (Msumbiji), MPLA (Angola), SWAPO (Namibia),

ZANU- PF (Zambia) CCM wenyeji kila chama kimetoa washiriki 20 pamoja na CPC ambaye ni mfadhili mkuu.


Related Posts