‘Mageuzi makubwa sekta ya ardhi yanakuja’ Waziri Silaa

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa amesema Mageuzi makubwa Sekta ya ardhi yanakuja baada ya kushuhudia utiaji saini kati ya Wizara yake na Mtaalamu Mshauri wa Mradi Mkubwa wa Kuimarisha na Kuboresha Miundombinu ya Upimaji na Ramani (LDI) wenye thamani takribani Bil. 150 za kitanzania.

Waziri Silaa amebainisha kuwa Mradi huo utaongeza uwezo wa Wizara wa kuandaa ramani za msingi kwa nchi nzima ambazo licha ya kutumika katika kupanga matumizi ya Ardhi mijini na vijijini, pia zinahitajika kwa matumizi mengine mengi katika ujenzi wa miundombinu kama barabara, reli, njia za mawasiliano, pia katika ulinzi na udhibiti wa maliasili, madini, ikiwemo mazingira.

Jerry Silaa amesema hayo mapema leo Mei 9, 2024 wakati wa Hafla fupi ya utiaji Saini Mkataba wa kati ya Wizara na Mshauri Elekezi wa Mradi wa Kuimarisha Miundombinu ya Upimaji na Ramani Bw. Kim, Ki Hwan atakayesimamia utekelezaji wa mradi huo hafla iliyofanyika Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.

Mradi huu ukikamilika utawezesha huduma za ardhi za kuthamini, kupanga, na kupima kufanyika kwa haraka na kwa gharama nafuu sana, hivyo kufanikisha azma ya Serikali ya kupima kila kipande cha ardhi nchini.

Waziri Silaa aliongeza kuwa Mradi huu Mradi huu una vipengele vikuu vinne ambavyo ni Kuandaa ramani za msingi ambazo zitandaliwa katika Miji mikuu ya Mikoa 26 nchini yakiwemo Majiji na Manispaa zote na kuongeza kuwa mradi pia utaandaa ramani ya uwiano mdogo kwa nchi nzima.

Related Posts