Ukatili wa kijinsia wapungua Mara

Na Malima Lubasha, Tarime

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum, Dk.Doroth Gwajima amesema Mkoa wa Mara umeendelea kupiga hatua katika kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ukiwemo ukeketaji ambao umeshuka hadi asilimia 28 kutoka nafasi ya kwanza kama ulivyokuwa hapo awali.

Dk.Gwajima ameitaja mikoa ya Arusha na Manyara kuwa ndiyo inaongoza hapa nchini katika ukeketaji kwa kufungana kwa kuwa katika asilimia 43.

Waziri Dk.Gwajima amesema hayo Desemba 9, 2024 katika kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kitaifa zilizofanyika uwanja wa Shule ya Sekondari Ingwe ,Nyamongo wilayani Tarime mkoani Mara.

Amesema kuwa wadau mbalimbali kutoka Serikalini,Taasisi za dini,Mashirika ya KIraia,Wazee wa Mila na Wananchi wameshiriki katika kilele hicho chini ya kauli mbiu ya mwaka huu usemao ‘ Kuelekea miaka 30 ya Beijing Chagua Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia’.

Aidha Dk.Gwajima amesema Mkoa wa Mara kwa sasa umeendelea kupiga hatua tofauti na hapo awali ambapo vitendo hivyo vilikuwa vimeshika kasi na kuhimiza wananchi kuendelea kuachana na mila na vi tendo vinavyochochea vitendo hivyo vinavyorudisha nyuma shughuli za maendeleo.

“ Vitendo vya ukeketaji mkoani Mara umeendelea kupungua kwa mujibu wa Tafiti za Kitaifa za idadi ya watu na Afya Tanzania za mwaka 2022, ambapo mkoa wa mara una asilimia 28,maeneo mengine umesh uka asilimia 2 mengine umepanda ,Wakati Mkoa wa Arusha una asilimia 43,Manyara asilimia 43,Singida asilimia 20,Tanga asiliia 19,na Dodoma asilimia 18 hivyo napongeza mkoa wa mara kuendelea kufanya juhudi zaidi kupunguza kiwango cha ukeketaji,”amesema Dk.Gwajima

Pia amesisitia mambo ya ukatili mwingine tuanze kuondoa Mara sura ya ukatili wameitikia pasipo na shaka kwa sababu ya viongozi wenu wakuu wote wameshirikiana pamoja na jamii na wazee wetu wa kimila.

Hata hivyo Waziri Gwajima ameyataka mashirika ya kiraia na wadau wa kupambana na ukatili wa kijinsia kuendelea kutoa elimu hasa kwa wanawake wanaoishi vijijini kwani ndiko idadi kubwa ya vitendo vya uk atili vimekuwa vikifanyika na serikali itazidi kushirikiana na taasisi zote za jamii kujenga Taifa imara lisilo na vitendo vya ukatili.

Amewashukuru wazee wa kimila kutoka koo 12 za kabila Wakurya kuendela kuiunga mkono serikali kupiga vita vitendo vya ukatili amewahimiza na kuwataka kutoa elimu zaidi katika jamii akisema madhara ya ukatili yanarudisha nyuma jitihada mbalimbali za maendeleo na kuhatarisha afya, usalama wa wanawake hasa wanaokumbana na ukeketaji,vipigo na ndoa za utotni na ukatili mwingine.

Naye Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini,Mwita Waitara amesema ili kumaliza la ukeketaji ni lazima elim u inayotolewa iwe shirikishi kutokana na jambo hilo kuwa ni la kimila na pia mfumo dume bado upon a kukiri kuwa ukatili kwa sasa umepungua kwani awali matukio mengi ya ukatili yalishamiri na wakati mwingine yalifanywa hadharani.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara, Apolinary Lyambiko amesema mgodi huo umekuwa ukifanya jitihada mbalimbali kuwezesha suala la usawa wa kijinsia mahala pa kazi kutokana na dhana iliyojengeka katika jamii kuwa sekta ya madini ni ya wanaume pekee.

“Mgodi umefanikiwa kuwa na ongezeko la watumishi wanawake kwa asilimia 4.8 katika kipindi cha mia ka mitatu iliyopita,ambapo hivi sasa mgodi wetu una watumishi wanawake 461 sawa na asilimia 12.8kati ya watumishi 3,613 hii yote inatokana na jitihada za makusudi zinazofanywa na mgodi katika kuboresha na kuweka mazingira rafiki kwa wanawake kujiunga na Kampuni yetu,”amesema Lyambiko

Lyambiko amesema pia mgodi huo umekuwa ukitekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ina yolenga kuboresha masuala ya usawa wa kijinsia katika jamii kama ujenzi wa mabweni kwa wasichana na wodi za wanawake ambapo katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita mgodi huo umetekeleza miradi 253 yenye thamani zaidi ya shilingi bilioni 22.

Related Posts