DC MPOGOLO ATOA NENO KWA WAJUMBE KAMATI ZA MIKOPO NGAZI YA KATA

 Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amewataka wajumbe wa kamati ya huduma ya mikopo  ngazi ya kata  kuhakikisha wanakuwa vinara wa ukusanyaji marejesho ya Mkopo wa asilimia kumi wa jiji.

Mpogolo ameyasema hayi jijini Ilala, Mkoani Dar es salaam wakati  anazungumza katika hafla ya uapisho wa uwajibikaji  na uadilifu katika  utoaji na usimamizi wa mikopo ya asilimia kumi kwa wajumbe wa kamati ya huduma ya mipoko ngazi ya kata.

Mpogolo  amesema kuwa  wajumbe wa kamati hizo wawe na uadilifu na ufuatiliji wa makusanyo ya mkopo ya asilimia kumi kwa awamu ya pili ambapo halmashauri ya jiji la Ilala limetenga kiasi cha shilingi bilioni 14. 085  za fedha zitazoanza kutolewa kwa wakopaji hivyo  halmshauri  ya ilala ihakikishe inakuwa vinara kwa wataonufaika.

Ameongeza kuwa Rais Dokta Samia Suluhu Hassan awali aliona changamoto za mikopo awamu ya kwanza na makusanyo madogo  na kuhamasisha halmashauri nyingi kuongeza makusanyo.

Hali iliyofanya utolewe utaratibu mzuri wa kushirikisha ngazi za chini kabisa serikalini katika utoaji mikopo hivyo kuwataka wajumbe wa kamati hiyo  walioapishwa kutenda haki kuhakikisha mikopo inafika kwa walengwa. 

Katika hafla hiyo wajumbe hao wa kamati wamekabidhiwa vipaza sauti ambavyo ni  vitendea kazi vya kutolea elimu ya mikopo kwa kata zote 36 za halmashauri ya Jiji la Ilala.

Aidha Mpogolo ametumia hafla hiyo kuonya baadhi ya tabia ya watendaji wasio waadilifu katika mikopo hiyo kuomba kiasi cha fedha, kuingiza ndugu zao na marafiki bila utaratibu jambo linalofanya wanufaika wasipate nafasi ya kupata mikopo. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa jiji la Ilala Elihuruma Mabelya amesema wako tayari kuhakikisha mikopo inatolewa kwa walengwa wenye sifa ili wawe wanufaika wa mikopo ya asilimia kumi kwa awamu ya pili.

Huku akieleza mafanikio ya agizo la Mkuu wa wiliaya hiyo Edward Mpogolo kuwataka kufuatilia madeni ya mikopo iliyopita ambapo ameeleza hadi sasa wamekusanya kiasi cha shilingi  milioni themanini na zoezi linaendelea.

Related Posts