Kampeni ya msaada wa kisheria yazinduliwa rasmi Iringa

Uzinduzi wa Kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria kwa wananchi ya Mama Samia Legal Aid umefanyika rasmi Mkoani Iringa katika uwanja wa Mwembetogwa uliopo Manispaa ya Iringa ambapo wananchi wameaswa kujitokeza kupata huduma za kisheria katika masuala yanayowasumbua.

Mgeni rasmi katika shughuli hiyo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Iringa amewasisitiza Wananchi katika maeneo mbalimbali ambapo Kampeni hiyo itafika kujitokeza ili kupatiwa msaada wa kisheria katika masuala yanayowakabili kwani ndio lengo la kampeni hiyo.

“Lengo letu ni kuhakikisha kuwa kila Mwananchi hasa wanawake na watoto wanapata haki zao na msaada wa kisheria bila vikwazo, kampeni hii ni sehemu ya utekelezaji wa malengo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha kuwa huduma za kisheria zinapatikana kwa wote, na kwamba wananchi wanapaswa kuwa na ujasiri wa kudai haki zao bila woga”, amesema Ngwada.

Kampeni hiyo inatekelezwa kwa ushirikiano na Taasisi mbalimbali za kisheria na asasi za kiraia, ambazo zitakuwa na jukumu la kutoa huduma za kisheria bure kwa wananchi katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huku ikiongozwa na kauli mbiu ya

“Msaada wa Kisheria kwa Haki, Usawa, Amani na Maendeleo”.

Related Posts