Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Insurance Kaimu Mkeyenge akikabidhi sehemu ya msaada wenye thamani ya sh.Milioni 10 Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele Kwa ajili ya Waathirika wa Mafuriko wa Kata 13 za Wilaya hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Insurance Kaimu Mkeyenge akizungumza mara baada ya kukabidhi sehemu ya msaada wenye thamani ya sh.Milioni 10 kwa ajili ya Waathirika wa Mafuriko wa Kata 13 za Wilaya ya Rufiji.
Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Insurance Kaimu Mkeyenge akishikana Mkono na Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele mara baada ya kukabidhi sehemu ya msaada wenye thamani ya sh.Milioni 10 kwa ajili ya Waathirika wa Mafuriko wa Kata 13 za Wilaya ya Rufiji.
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV Rufiji
NIC Insurance imetoa msaada vyakula na mahitaji ya msingi vyenye thamani ya Sh.Milioni 10 kwa waathirika mafuriko katika Kata 13 za Wilaya ya Rufiji.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Insurance Kaimu Mkeyenge amesema msaada huo ni kutoa faraja kutokana mafuriko waliyoyapata.
Amesema kuwa msaada walitoa kama Taasisi wameguswa na kutaka Taasisi zingine zilizo za Serikali na zile zilizo kuwa za Serikali kuona kuna jambo la kufanya kwa waathirika mafuriko Wilaya ya Rufiji.
Mkeyenge amesema kuwa katika mazingira ya kawaida wananchi waliokumbwa na mafuriko wanahitaji msaada kutokana na wao kupoteza kila kitu.
Aidha amewakumbusha wakulima na wafugaji kukata bima za kilimo na mifugo ili wakati wa maafa waweze kupata fidia ya hasara waliyopata na kuendelea na maisha yao kama kawaida.
Hata hivyo ameipongeza Serikali kwa hatua zilizochukuliwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kutoa msaada mara moja pindi mafuriko yalipokea.
Mkeyenge amesema kuwa katika hatua zilizochukuliwa ni pamojà na Viongozi Mkoa na Wilaya wamefanya kazi kubwa katika kutengeneza mazingira ya walioathirika kuwaweka sehemu salama.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele ameishukuru NIC Insurance msaada huo na kutaka wadau wengine kuguswa katika kuwasaidia sehemu ya wananchi wenzetu.
Amesema kuwa idadi ya walioguswa na mafuriko hayo ni watu 89OOOkwa kaya 623 ambazo haiwezekani kurudi katika makazi hayo.
Amesema kuwa waathirika hao hawatarejea katika makazi Yao ambapo kuna maaneo wameshatenga Kwa ajili yao wafanye Ujenzi wa makazi salama.