TANZANIA, UMOJA WA ULAYA WASAINI TAMKO LA KUUNGA MKONO JITIHADA ZA MAENDELEO

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Cosato Chumi akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo baada ya kusainiwa kwa tamko la makubaliano ya kuendelea kuunga mkono jitihada za maendeleo Desemba 10, 2024 jijini Dar es Salaam.

………………………………………..

Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Umoja wa Ulaya zimesaini Tamko la makubaliano ya kuendelea kuunga mkono jitihada za maendeleo kwa faida za pande zote mbili.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Cosato Chumi akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo baada ya kusainiwa kwa tamko hilo Desemba 10, 2024 jijini Dar es Salaam alisema ushirikiano huo ni wa muhimu sana.

“Majadiliano haya ya leo ni sehemu ya utekelezaji wa Mkataba wa Samoa, uliosainiwa mwaka 2023, ambao unaelekeza umuhimu wa kuwa na majadiliano ya mara kwa mara kati ya Umoja wa Ulaya na Nchi za Afrika, Karibiani, na Pasifiki (ACP). “ alisema.

Alisema Tanzania ni moja ya nchi wanachama wa kundi la ACP, ambayo inaendelea kutekeleza wajibu wake kwa kushiriki kikamilifu kwenye majadiliano hayo muhimu kila mwaka kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kimkakati na Umoja wa Ulaya.

Chumi alisema majadiliano hayo yalijielekeza zaidi katika masuala yanayogusa maslahi ya pande zote, ikiwa ni pamoja na utawala bora, demokrasia, usalama wa baharini, biashara na uwekezaji, na ulinzi na usalama kikanda na kimataifa.

Chumi alitaja baadhi ya maazimio yaliyofikiwa kwenye mkutano huo ambapo alisema kuwa Tanzania na Umoja wa Ulaya zimedhamiria kuimarisha zaidi ushirikiano wa pande mbili chini ya Mkataba wa Samoa. Ushirikiano huo unaendana na Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2020- 2025 na Mpango wa Tatu wa Maendeleo ya Miaka Mitano ambapo pande zote mbili zimekubaliana kuongeza ushirikiano ili kuhakikisha matokeo chanya na yenye manufaa kwa wananchi.

Aidha Chumi kwa niaba ya Tanzania akizungumzia ushirikiano wa maendeleo liushukuru Umoja wa Ulaya kwa msaada wake endelevu kupitia mfumo wa mpango wake wa maendeleo wa majirani na ushirikiano wa wa kimataifa ambao umeweka Uro 726 Milioni kwa Tanzania.

Alisema fedha hizo zimewezesha kutekeleza miradi muhimu katika sekta ya nishati , uchumi wa buluu, mabadiliko ya tabia nchi na mpango wa miji kuwa ya kijani.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia Kanda ya Afrika katika Kurugenzi ya Huduma za Nje ya Umoja wa Ulaya (Europeana External Action Service), Balozi Ritha Maria Laranjinha alihimiza kudumisha ushirikiano huo kwa ajili ya maslahi mapana ya wananchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia Kanda ya Afrika katika Kurugenzi ya Huduma za Nje ya Umoja wa Ulaya (Europeana External Action Service), Balozi Ritha Maria Laranjinha alihimiza kudumisha ushirikiano huo.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Cosato Chumi akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo na Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia Kanda ya Afrika katika Kurugenzi ya Huduma za Nje ya Umoja wa Ulaya (Europeana External Action Service), Balozi Ritha Maria Laranjinha wakisaini Tamko hilo la makubaliano.

Tamko hilo likisainiwa

Viongozi hao wakionesha tamko hilo baada ya kusainiwa.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Cosato Chumi, akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia Kanda ya Afrika katika Kurugenzi ya Huduma za Nje ya Umoja wa Ulaya (Europeana External Action Service), Balozi Ritha Maria Laranjinha.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Cosato Chumi, akimkabidhi zawadi Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia Kanda ya Afrika katika Kurugenzi ya Huduma za Nje ya Umoja wa Ulaya (Europeana External Action Service), Balozi Ritha Maria Laranjinha.
Wajumbe wa Umoja wa Ulaya wakiwa kwenye kikao hicho.

Related Posts