Fadlu ashtuka, aweka msimamo | Mwanaspoti

HUKO mtaani kwa sasa mashabiki wa Simba wanatambia mziki wa kikosi walichonacho, lakini kwa kocha Fadlu Davids hali ni tofauti kwani, ameshtukia jambo analoamini likifanyiwa kazi linaweza kuifanya timu hiyo itishe zaidi, huku akiweka msimamo wake kabla ya kukabiliana na CS Sfaxien ya Tunisia.

Simba inayoshika nafasi ya pili kwa sasa katika Ligi Kuu Bara na iliyopo makundi ya Kombe la Shirikisho, ambapo Jumapili itashuka uwanjani kukabiliana na Watunisia katika mechi ya tatu ya Kundi A itakayopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Sasa kama ulikuwa unadhani Simba imejipata kutokana na rekodi bora ilizonazo katika michuano ya ligi basi umekosea, kwani kocha Fadlu amefunguka kuwa eneo la ushambuliaji bado linampasua kichwa, huku akiwataja Leonel Ateba na Steven Mukwala wanatakiwa kubadilisha mambo ili Simba itishe zaidi nje ndani.

Simba ambayo inashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho iko kundi A imecheza mechi mbili mpaka sasa ikishinda dhidi ya Bravos ya Angola bao 1-0 na CS Constantine 2-1.

Huku katika ligi ikiwa nafasi ya pili ikiwa imecheza mechi 11,ikishinda tisa,sareĀ  na kupoteza moja sawa na alama 28.

Msimu huu Simba imefanya usajili mzito msimu, huku kila eneo likiwa na mastaa wapya wenye rekodi za maana tu na miongoni mwao Mukwala na Leonel Ateba.

Akizungumza na Mwanaspoti Fadlu alisema kuwa, amepanga na kupangua safu yake ya ushambuliaji lakini bado timu yake inahitaji kuongezewa nguvu.

Alisema kuwa, anahitaji mshambuliaji mwenye njaa ya mabao na kushinda Ateba na Mukwala bado wamekuwa wanakosa muendelezo wa makali yao, lakini wao kama makocha hawajachoka kuendelea kuwabadilisha

“Bahati mbaya ni kwamba washambuliaji wako wachache sana na tunaingia kwenye dirisha dogo ambalo sio uhakika kuweza kupata watu Bora zaidi.

Changamoto yao kubwa ni kwamba hawakupi kile uachotaka kila muda,kwani wamekosa muendelezo wa makali yao hasa katika mechi muhimu.”

Aliongeza kuwa: “Kama makocha hii ni kazi yetu kubadilisha wachezaji wawe katika viwango bora, lakini inapokuja tunaposhiriki michuano mikubwa kama hii kinachohitajika ni wachezaji waliobora zaidi na wenye kiu ya mafanikio kwaajili ya yao na timu kwa ujumla.”

Simba msimu uliopita iliwaacha mastaa wenye rekodi nzuri za ufungaji kama Jeans Baleke mabao (7),Saido Ntibazonkiza (7),Freddy Kouablan (5) na Clatous Chama(7), huku wengi kati yao wakiwa na uzoefu wa kucheza michuano ya ligi na kimataifa.

Ni wazi kuwa maingizo mapya hasa eneo la washambuliaji limeonekana bado likijitafuta kwani katika michuano ya kimataifa Simba ilianza na Mukwala mechi ya kwanza na Ateba ya pili,huku wakiwa hawajatia kambani bao lolote kati ya mawili yaliyofungwa.

Katika mchezo wa kwanza bao lilifungwa na kiungo Charles Ahoua na wa pili uliochezwa ugenini na ilipoteza kwa 2-1 mfungaji akiwa beki Mohamed Hussein, hivyo ni wazi kuwa eneo hilo bado linajitafuta.

Katika mabao 16 iliyofunga Simba katika michuano ya ligi nako washambuliaji wamekuwa nyuma kwani rekodi zinaonyesha kuwa:

Simba ina washambuliaji watatu ambao ni;

Simba itaingia Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumapili Desemba 15 kukichapa dhidi ya SC Sfaxien ya Tunisia, ikiwa ni mchezo wa tatu hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Afrika.

Related Posts