Manahodha wakikabidhiwa bendera ya Chuo, na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakati wa halfa ya kuwaaga.
…..
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Prof. Razack Lokina, leo tarehe 13 Desemba, 2024 amewaaga Wanafunzi 57 ambao wanatarajia kushiriki Mashindano ya Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki ambayo kwa mwaka huu yanafanyika Kisumu nchini Kenya, kuanzia tarehe 14 hadi 21 Desemba 2024.
Prof. Razack Lokina amewataka Wanafunzi hao pindi watakapokuwa kwenye Mashindano hayo wazingatie nidhamu na kurudi na ushindi kama ilivyo desturi ya UDOM.
” Msirudi mikono mitupu mpambane, ndo maana tumewapatia mahitaji yote mnayohitaji; tukatangaze nchi yetu maana mmeshikilia bendera mbili ya Taifa na UDOM”. Alisisitiza
Naye Mkufunzi wa Michezo Bw. Deogratius Mdemu, amesema michezo inayokwenda kushindaniwa ni Mpira wa Miguu wanawake na wanaume, mpira wa Wavu, Mpira wa Pete na mchezo wa Walemavu “Mpira wa Wasioona “Goal ball”
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof. Razack Lokina, akimkabidhi vifaa vya michezo nahodha wa timu ya mpira wa pete, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika Jengo la Benjamin Mkapa, Dodoma.
Manahodha wakikabidhiwa bendera ya Chuo, na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakati wa halfa ya kuwaaga.
Kikosi cha wachezaji wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya hafla ya kuwaaga iliyofanyika makao makuu ya chuo hicho Dodoma