MHE. MCHENGERWA NI ‘ASSET’ YA RUFIJI NA TAIFA

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Dkt. Festo Dugange amewaambia wananchi wa Jimbo la Rufiji kuwa Mhe. Mohamed Mchengerwa ni ‘Asset’ ya Jimbo la Rufiji na Tanzania kwa ujumla kutokana na utendaji kazi wake unaogusa kila sekta muhimu kwa watanzania.

Mhe. Dugange ameyasema hayo wakati akitoa salaam zake kwa wananchi wa Wilaya ya Rufiji kwenye ufunguzi wa Tamasha la Bibi Titi Mohamed uliofanyika kwenye uwanja wa Ujamaa Ikwiriri leo 13.12.2024.

Amesema Mhe. Mchengerwa ni Mbunge wa Rufiji na amefanya kazi kubwa katika Wilaya hiyo kuanzia kwenye sekta ya Afya, Elimu, miundombinu ya barabara na kuinua wananchi kiuchumi huku pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI na kwamba aliyoyafanya Rufiji ameyafanya kwenye Halmashauri zote nchini ni muhimu hkumlinda na kumuombea kwa utendaji kazi wake.

Related Posts