PROFESA Kitila Mkumbo aliyewahi kuwa kiongozi mwandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) baadaye ACT Wazalendo na sasa ni Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema kuwa Tundu Lissu ameudanganya umma kuwa yeye na Zitto Kabwe Kiongozi Mstaafu wa ACT walikuwa wanapanga mipango ya kumpindua Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chadema. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Profesa Kitila akijibu maswali ya waandishi wa Habari leo tarehe 13 Desemba, 2024 alisema kuwa mapinduzi hayawezekani kwenye chama cha siasa kwa sababu hakuna mifumo ya kijeshi.
“Lissu ni mwanasheria anafahamu kuwa mapinduzi yanafanywa katika nchi sasa katika chama cha siasa utapindua kwa jeshi lipi hauna silaha kama nilivyowahi kusema yalikiwa mapambano ya kidemokrasia na hawakuwa tayari kwa Demokrasia,” alisema Prof. Kitila.
Amesema kuwa mapambano anayopambana Lissu leo, wao waliyapambana yeye na Zitto miaka 13 iliyopita, ilhali Lissu alitumiwa na Mbowe kama silaha ya kuwamaliza kisiasa yeye na Zitto.
“Hakuna utaratibu wa tofauti sisi tulikuwa tunajiandaa kama alivyofanya yeye jana kwenda kupambana na mwenyekiti aliyekuwepo kama alivyofanya yeye na Msigwa,” alisema Prof. Kitila.