Na Mwamvua Mwinyi, Pwani Mei 9
Mkuu wa Dawati la elimu ya usalama barabarani Tanzania Kamishina Msaidizi wa Polisi, Michael Deceli , ametoa rai kwa madereva walioweka magari yao ving’ora pasipo kuwa na kibali cha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, kuondoa mara moja kwani ni kinyume na uta.
Aidha amewataka madereva wa vyombo vya moto kuzingatia alama za barabarani ili kupunguza ajali kwa watumiaji wengine wa barabara.
Deceli ameitoa rai hiyo, baada ya kuhitimisha utoaji wa elimu ya uvukaji wa barabara kwenye vivuko vya waenda kwa miguu kwa wanafunzi wa shule ya msingi Misugusugu Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani.
“Suala la kuheshimu alama za barabarani ni la kila dereva anayeendesha chombo cha moto, Sheria haijabagua madereva wa kuziheshimu alama hizo na wengine kutokuheshimu”.
Deceli ametaka kila dereva afuate sheria na alama zilizopo kwa usalama wa barabarani.