Uzinduzi wa Madini ya Vito Wafanyika Mji mdogo wa Mererani Wilayani Simanjiro,Mkoani Manyara.

 

Na Jane Edward, Manyara

Serikali imesema haina mpango wa kuchukua madini ya wafanyabiashara wa madini yatakayobaki kwenye minada itakayokuwa inaendeshwa na kusimamiwa na wizara ya Madini.

Akizungumza Mkoani AManyara mji mdogo wa Mererani wakati wa zoezi la uzinduzi wa mnada wa madini ya vito, Waziri wa Madini Anthony Mavunde Mavunde amesema dhana potofu imejengeka miongoni mwa wafanyabiashara hao kutokana na mnada uliofanyika kipindi cha nyuma na kuchukuliwa kwa madini hayo.

Amesema kuwa madini hayo yapo mikono salama na tayari yameshachukuliwa kutoka Bank kuu ya Tanzania na kwamba muda sio mrefu yatarejeshwa kwa wafanyabiashara hao kwaajili ya kuuzwa kama ilivyokuwa hapo awali.

Akizindua minada ya ndani ya madini ya vito iliyofanyika leo katika mkoa wa kimadini Mirerani Manyara iliyowakutanisha wadau wa madini kutoka ndani na nje ya nchi amesema minada hiyo inaendeshwa na Tume ya madini kwa kushirikiana na soko la bidhaa Tanzania (TMX) kupitia mfumo wa mauzo wa kielektroniki ili kuweka uwazi kwa wadau wote wa madini.

Amesema sekta ya madini imeendelea kukua na kuongeza fedha katika mfuko mkuu wa serikali kutoka shilingi bilioni 161 katika mwaka wa fedha 2015/2016 hadi kufikia shilingi bilioni 753 huku lengo ni kukusanya trilioni moja kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Mavunde amesema katika makusanyo ya fedha za mnada huo yanatokana na serikali kuweka udhibiti mzuri wa madini ya vito .

 Queen Sendiga ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara ambapo ametumia nagasi hiyo kuiomba serikali kuwatenganisha wafanyabiashara wadogo na wakubwa kwenye minada ya madini ili kuhakikisha kila kundi linafaidika na minada hiyo.

Aidha amesema kuwa utaratibu uliopo unawapa wakati mgumu kwani unasababisha washiriki wadogi wa minada hiyo kushindwa.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la  Simanjiro Christopher Ole Sendeka amemuomba Waziri Mavunde kushughulikia kero ya ukaguzi getini inayosababisha watu kutoka kuanzia saa saba hadi saa nane usiku kutokana na foleni kubwa ambapo Waziri walimuomba Mkuu wa Mkoa kushughulikia kero hiyo.

 

Related Posts