Meneja wa Uzalishaji Kampuni ya Tanlapia Farida Buzohera akilisha Samaki Chakula.
BENKI ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imesema inajivuni mradi wa kimkakati wa kuzalisha samaki aina ya Sato unaomilikiwa na kampuni ya Tanlapia ambapo umeleta mafanikiwa makubwa nchini na kuongeza ulaji wa samaki kwa wananchi.
Meneja wa Kanda ya Mashariki Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) Michael Madundoakizungumza mara baada ya waandishi wa bahari kutembelea mradi huo Desemba 13, 2024 amesema kuwa mradi huo wa kimkakati kwa sasa unazalisha Samaki tani 35 kwa mwezi na wanauza katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Iringa, Tanga na Mbeya.
Amesema TADB imefanikiwa kuiwezesha Kampuni hiyo kwa mtaji mbapo mpaka sasa imeshaa toa ajira kwa watu 116 jambo ambalo limeleta tija kwa Taifa.
Mradi huo wa Kampuni ya Tanlapia upo Kata ya Nia Njema, Wilaya ya Bagamoyo,
unatumia teknolojia ya kisasa ambayo inatumia maji kidogo na kuzalisha samaki wengi na kuleta ufanisi katika utendaji.
Mradi huo unasaidia kutekeleza majukumu ya Serikali kwa kuongeza utoshelezaji wa chakula nchini, kwani mahitaji ya chakula hasa samaki kwa mwaka tani laki tatu.
Madundo ameeleza kuwa ulaji wa samaki nchini upo chini ya wastani kwani mtu mmoja anakula kilo sita hadi saba kwa mwaka badala ya kula kilo 20 kwa mwaka.
”Bado hatupati protini ya kutosha, hivyo mradi huo unavyotekelezwa unaweza kutusongeza katika malengo ya Taifa kwa kuongeza utoshelezi wa chakula na kuhakikisha wananchini wanapata virutubisho vya kutosha” amesema Bw. Madundo.
Amesema kuwa mradi umeajiri wanawake pamoja na vijana, huku akieleza kuwa kadri muda unavyozidi kwenda wataendelea kutoa ajira hasa kwa wananchi wanaoishi katika Wilaya ya Bagamoyo.
Kwa upande wa Meneja wa Uzalishaji Kampuni ya Tanlapia Farida Buzohera, amewapongeza TADB kuwa kuwawezesha kiuchumi kwa kufanya maboresho ya miundombinu ya uzalishaji wa samaki.
Amesema kuwa kupitia uwezeshaji huo wamefanikiwa kupiga hatua na kuzalisha tani 35 za samaki kila mwezi, huku akieleza mpaka kufikia mwaka 2025 wanatarajia kuzalisha tani 100 kwa mwezi.
Amesema kuwa mafanikio waliopata yametokana na ushirikiano mkubwa kutoka benki ya TADB, Benki ya CRDB pamoja na wadau kwani awali walikuwa wanazalisha kiasi kidogo cha samaki
.
“Kuna upungufu wa samaki Ziwa Victoria, Bahari ya India, hivyo kuna ukosefu mkubwa wa protini kwa ujumla nchini, hata ukifikia uzalishaji wa tani 100 hatuwezi kukizi mahitaji ya wananchi wote, tunaendelea kuongeza idadi ya uzalishaji kila mwaka.” Amesema Farida
Amesema kuwa Tanlapia inafanya kazi kubwa ya uzalishaji wa vifaranga vya samaki, ukuzaji pamoja na kuuza wa samaki wakubwa, huku akifafanua kuwa samaki wanaozalisha na kuingia sokoni ni wakubwa ambapo watatu sawa na kilo moja.
“Uzalishaji wa samaki mpaka inamfikia mraji inachukua muda wa miezi tisa hadi 11, na tunauza kwa bei rafiki lengo ni kuhakikisha kila mtazania anapata protini kupitia samaki.” Amefafanua Farida