Waziri Ndumbaro aongoza zoezi la kutoa msaada wa kisheria kwa gereza la kiberege kwa wafungwa na Mahabusu

Waziri wa katiba na Sheria Dokta Damas Ndumbaro ameongoza zoezi la kutoa msaada wa kisheria kwa wafungwa na mahabusu Gereza la Kiberege lililopo Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro.

Dk. Ndumbaro atoa msaada huo katika uzinduzi wa kampeni ya Mama Samia Legal Aid Wilayani humo ambapo amesema lengo la Kampeni hiyo ni kusaidia Wananchi katika utatuzi wa masuala ya kisheria.

Amesema Serikali inatambua haki ya kila mtu hivyo msaada huo wa kisheria utamfukia kila mtu Ili aweze kupaata haki yake ya kisheria.

Aidha Dokta Ndumbaro amesema Kampeni hiyo ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia tiyari imewafikia wakazi wa mikoa 11 na kwa Mkoa wa Morogoro

itafika Wilaya Zote za Mkoa pamoja na kata zake Ili wananchi wa vijijini nao waweze kunufaika .

Waziri Ndumbaro ameongeza kuwa Serikali Kwa kushirikiana na chama Cha mawakili Tanganyika (TLS)inajipanga kuanzisha kambi maalum ya mawakili watakaotembelea mageraza zote nchini Kwa ajili ya kutoa elimu ya msaada wa kisheria Kwa wafungwa na mahabusu.

Akizungumza na Ayo tv na Millard Ayo .com Mmoja wa wakazi wa Kilombero ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria kwa Kuja na kampeni hiyo ambayo imetajwa kuwa mkombozi hasa Kwa wananchi wa hali ya chini.

Anasema licha ya kupata nafasi ya kutatuliwa changamoto zao lakini pia wanapata elimu ya masuala mbalimbali ya kisheria ambayo awali yalikuwa kikwazo katika ufunguaji wa mshauri mahakamani.

 

Related Posts