PICHA: Matukio ya vurugu Kwa Mkapa, Simba Vs CS Sfaxien

Picha za matukio mabalimbali ya vurugu baada ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika uliowahusisha wenyeji Simba SC dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia uliochezwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam jana Desemba 15, 2024.

Mchezo huo uliisha kwa timu ya Simba kushinda kwa mabao 2-1, Wekundu wa Msimbazi wakipata bao dakika za jioni (90+) likifungwa na Kibu Denis kitendo kilichowafanya wachezaji na mashabiki wa CS Sfaxien kutoridhishwa na mwamuzi wakionyesha kuamini kwamba mchezo ulikuwa umekwisha na kuanzisha vurugu.

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam baada ya vurugu hizo lilitoa taarifa kuhusu uharibifu uliofanyika likisema jumla ya viti 256 viling’olewa.

P 01

“Kulitokea fujo iliyosababishwa na mashabiki wa Timu ya CS Sfaxien kutoridhika na maamuzi ya refa wa mchezo huo kuchezesha mechi hiyo kwa zaidi ya dakika saba ambazo aliziongeza kama dakika za nyongeza jambo lililopelekea timu ya Simba kupata goli la pili na la ushindi.

Wachezaji wa ndani ya uwanja na “benchi” la ufundi la timu ya CS Sfaxien walikasirika, wakamfuata mwamuzi wa mchezo na kuanza kufanya vitendo vya kumshambulia.

“Katika fujo hizo shabiki mmoja wa timu ya CS Sfaxien aliumia na kupatiwa huduma ya kwanza na kuruhusiwa, huku viti vya rangi ya blue 156 na Orange 100 viling’olewa na mashabiki hao,” imesema taarifa hiyo ya polisi.

P 02

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ilieleza wizara imesikitishwa na vitendo vya mashabiki kung’oa na kuharibu viti vya kukalia watazamaji kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Na kwamba Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Palamagamba Kabudi amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Gerson Msigwa kuchukua hatua mara moja kwa kuwaandikia timu ya Simba Sports Club na kuwanakili Shirikisho la Kandanda Tanzania (TFF) ili gharama za uharibifu uliosababishwa wakati mechi hiyo zilipwe.

P 03
P 04
P 05
P 05

P 06
P 07
P 08
P 09
P 10

Related Posts