DKT. NCHEMBA ZIARANI OMAN APONGEZA DIPLOMASIA YA UCHUMI


Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (mwenye skafu), Balozi wa Tanzania nchini Oman Mheshimiwa Fatma Rajab (wa tano kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Tanzania baada ya kuhitimisha mazungumzo yao katika Makazi ya Balozi, nchini Oman.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Oman).

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akizungumza na watumishi wa Ubalozi wa Tanzania Muscat- Oman na wadau wengine katika Makazi ya Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Fatma Rajab, ambapo Mhe. Dkt. Nchemba yuko nchini humo kwa ziara ya kikazi. Amempongeza Mhe. Balozi Fatma Rajab kwa kazi kubwa na njema ya kueneza diplomasia ya kiuchumi nchini humo kwa mafanikio makubwa.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Oman Mheshimiwa Fatma Rajab, akizungumza wakati alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Ubalozi huo, katika Makazi yake, Mjini Muscat-Oman. Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu, yuko katika ziara ya kikazi nchini humo.
Kamishna wa Idara ya Sera Wizara ya Fedha, Bw. Johnson Nyella, akifafanua jambo wakati wa mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), na Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Fatma Rajab, mazungumzo yaliyofanyika katika Makazi yake mjini Muscat-Oman.
Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha Bw. Robert Mtengule, akichangia mada wakati wa mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Fatma Rajab na watumishi wa Ubalozi huo na wadau wengine. Kushoto ni Kamishna wa Idara ya Madeni Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Sheria Wizara ya Fedha, Bw. Elias Kimati.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa pili kulia) akiongoza kikao alipoongoza Ujumbe wa Tanzania katika Makazi ya Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mheshimiwa Fatma Rajab.

Related Posts