Wahindisi wazuri wanatakiwa kutiwa moyo wa kuwa viongozi wazuri wa sasa na baadae

TAASISI ya Seris Foundation kwa kushirikiana na Smarcon Tanzania Limited na Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB) wameendesha warsha ya programu mpya za Kihandisi zilizoingia sokoni hivi karibuni kwa ajili ya kuongeza fursa za ajira na kujiajiri kwa Wahitimu wa fani ya Uhandisi.

Akizungumza katika kufunga warsha hiyo ya siku tatu Desemba 12-14, 2024, Injinia (Eng) Sudi Mwalimu amabye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Smarcon Tanzania Limited amebainisha kuwa, uongozi bora katika fani ya Uhandisi ni pamoja na kuwatia moyo washiriki katika fani hiyo ambao wengi wao wamehitimu na wapo mitaani.

Eng. Mwalimu amesema Wahindisi wazuri wanatakiwa kutiwa moyo wa kuwa viongozi wazuri wa sasa na baadae katika kujiajiri.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Seris Foundation, CPA Bi. Deborah Wami amesema mafunzo hayo yamefanyika vyema na kwa mafanikio huku wakiamini Mainjinia walioshiriki watafanya kazi zao kwa ufanisi zaidi ikiwemo Ujasiriamali baada ya kujifunza program hizo mpya za Kihandisi.

Kwa upande wao baadhi ya Washiriki wa Warsha hiyo, wamebainisha kuwa:
“Mafunzo haya yanaenda kutujenga katika Uhandisi hasa hii program mpya, lakini pia namna bora ya Uongozi katika Uhandisi.” Amesema mshiriki wa Warsha hiyo, Eng. Boniface Mwawengo

Eng. Diana Emmanuel ameishukuru Seris Foundation kwa mafunzo hayo na anaamini ameongeza maarifa katika taaluma yake aliyoisomea na kuahidi kuvifanyia kazi.

Related Posts