Simba yakiri kupokea maelekezo ya serikali, yapanga kuishitaki CS Sfaxien CAF

Klabu ya Simba imetoa taarifa baada ya tukio la jana la vurugu kwenye Uwanja wa Mkapa, mchezo wa hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia.

Simba imesema inasikitishwa na kulaani vurugu pamoja na uharibifu wa miundombinu katika michezo na inawakumbusha mashabiki kuendelea na kuwa na ukomavu na kutulia pale ambapo timu pinzani inapoanzisha fujo dhidi yao.

Pia imeongeza kuwa imepokea maelekezo ya serikali na itashirikiana na vyombo vya uchunguzi na mamlaka kufanya tathmini ya uharibifu uliotokea katika kadhia hiyo na itutaendelea kuwa klabu yenye kusimamia misingi, taratibu na sheria zilizowekwa kwa maslahi ya Taifa letu Ia Tanzania.

P 02

Imeongeza kuwa italiandikia Shirikisho la soka Afrika (CAF) juu ya kadhia hiyo iliyosababishwa na Timu ya CS Sfaxien ambayo imekua ni kinara wa matukio yasiyo ya kimchezo.

Soma zaidi Taarifa rasmi ya Simba hapa

Klabu ya Simba inapenda kutoa taarifa kwa umma kuwa, Tarehe 15 Desemba 2024, katika mchezo wake wa hatua ya makundi ya Kombe Ia Shirikisho Afrika dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia katika uwanja wa Benjamin Mkapa, zilizuka ghasia zilizoanzishwa na timu pinzani licha ya kupokelewa na kupewa ushirikiano mkubwa wa maandalizi na wao kusifia mapokezi na ukarimu wetu.

Mara baada mchezo kumalizika Wachezaji, Benchi la ufundi Ia CS Sfaxien pamoja na Viongozi wake walivamia uwanja na kuanza kuwashambulia waamuzi kitendo ambacho kilifanya wahudumu wa mechi (Stewards)  pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama (Polisi) kusaidia kuwaokoa waamuzi hao na kuwatoa uwanjani.

Klabu yetu haikubaliani na vurugu wala uharibifu wa miundombinu katika michezo na hivyo tunaomba na kuwakumbusha mashabiki wetu kuendeleza ukomavu wa kimichezo na kutulia pale ambapo timu pinzani zinapoanzisha fujo dhidi yetu.

Simba itashirikiana na vyombo vya uchunguzi na mamlaka kufanya tathmini ya uharibifu uliotokea katika kadhia hii na tutaendelea kuwa Klabu yenye kusimamia misingi, taratibu na sheria zilizowekwa kwa maslahi ya Taifa letu Ia Tanzania.

Simba Sports Club imeshiriki mara nyingi katika michezo ya kimataifa na kupelekea kupewa Tuzo ya Mashabiki Bora katika Mashindano ya Ligi ya Afrika, African Football League mwaka 2023.

Aidha tumepokea maelekezo ya Serikali na tunaliandikia Shirikisho la soka Afrika (CAF) juu ya kadhia hii kubwa iliyosababishwa na Timu ya CS Sfaxien ambayo imekua ni kinara wa matukio yasiyo ya kimchezo kwani nchini Tunisia Viongozi wao walidhalilisha waamuzi na kupelek-ea kufungiwa maisha kushiriki katika matukio ya mpira wa miguu, kufungiwa mara kadhaa kucheza bila mashabiki na kutozwa faini.

Tukio walilolifanya dhidi ya Waamuzi na Mashabiki wa timu yetu inao-nesha kuwa CS Sfaxien wamedhamiria kufanya fujo kwenye mpira kuwa sehemu ya utamaduni wao. Kuruhusu CS Sfaxien kuendelea kufanya matendo ya kihuni katika uwanja wa mpira ni kuhatarisha maisha ya Waamuzi, Wachezaji na Mashabiki. Klabu yetu inalaani vikali utovu uliofanywa na CS Sfaxien.

Related Posts