MKAZINGATIE VIPAUMBELE VYA TAIFA KATIKA MIPANGO NA BAJETI ZENU’ ENG. MATIVILA

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Miundombinu Mhandisi Rogatus Mativila amewataka Wataalamu wa Mipango na Bajeti kutoka kwenye Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuzingatia vipaumbele vya Taifa katika uandaaji wa mipango na bajeti zao.

Mhandisi Mativila ameyasema hayo wakati akifungua kikao kazi cha maandalizi ya Mpango na Bajeti kwa mwaka 2025/26 kwa Wataalamu toka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ofisi za Wakuu wa Mikoa Mamlaka za Serikali za Mitaa kinachofanyika Jijini Dodoma.

Amesema kikao kazi hicho kimelenga kuongeza uelewa kwa wataalamu hao ili kuandaa Mipango na Bajeti za Mikoa na Halmashauri zinazoakisi fursa zilizopo katika maeno hayo ili kuboresha Maisha ya wananchi.

Aidha ameelekeza kikao kazi hicho kuangalia kwa kina mambo mbalimbali katika maandalizi ya upangaji wa Bajeti ya mwaka 2025/26 ikiwemo rasimu ya Dira ya Taifa ya mwaka 2020 – 2050, kujadili vipaumbele vya Taifa, biashara ya hewa ya kaboni, mwongozo uendeshaji makapuni mahususi (SPV) kwajili ya kuanzisha na kusimamia miradi ya vitega Uchumi vya Halmashauri na namna ya kuingia ubia na kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP centre).

Related Posts