MFUMO WA KODI ULIOPO NCHINI UNARUHUSU KUWEPO UTITIRI WA KODI NYINGI ZINAZOSIMAMIWA NA MAMLAKA TOFAUTI

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mh. Othman Masoud Othman, amesema kwamba mfumo wa Kodi uliopo nchini unaruhusu kuwepo utitiri wa kodi nyingi zinazosimamiwa na mamlaka tofauti jambo linaloweza kusababisha kuanguka biashara kutoka kwenye sekta mbali mbali nchini.

Mhe. Othman ameyasema hayo huko ofisini kwake Migombani mjini Zanzibar alipokutana na Tume ya Rais ya kuangalia mfumo wa Kodi ndani ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mwenyekiti wake Balozi Ombene Sefue.

Aidha mhe. Makamu amesema kwamba kuwepo mamlaka nyingi za kodi mbali na kusababisa usumbufu kwa wafanyabiashara nchini lakini ni changamoto kubwa ambayo ni muhimu kwa tume iyo kuangaliwa upya jambo hilo hasa katika sekta makhususi za kiuchumi ikiwemo usafiri wa anga na huduma katika sekta ya kilimo.

Amefahamisha kwamba kutokana na hali hiyo kuna haja kubwa kwa Tanzania kubadili mwelekeo wa mfumo wa kodi ndani ya nchi ili kurahisisha shughuli za kodi na biashara ili ziweze kwenda kwa wepesi zaidi kuliko ilivyo sasa .

Aidha Mhe. Amesema kwamba licha ya taifa kujitaidi katika kukuza sekta mbali mbali ni vyema kuangalia mfumo sahihi wa kodi za kisekta kama vile kilimo jambo litakalochangia rasilimali zilizomo kuweza kuwekezwa na kuleta tija ndani ya Tanzania.

Mhe. Othman ali livyo sasa inaweza kuchania baadhi ya wafanyabiashara kushindwa sio tu kulipa kodi kikamilifu na nchi ikapata tija, lakini kutoendelea na shughuli za kibiashara jambo linalohita kuangaliwa kwa makini.

Akizungunzia suala la kodi katika sekta ya usafirishaji wa anga Mhe. Othman, amesema kwamba Tanzania imeshawahi kuwa na kampuni nyingi ambazo utoa fursa nyingi za ajira lakini bodo ni eneo linaloitaji kurekebsiwa zaidi katika mfumo wa kodi ili liweze kusaidia tija zaidi kwa manufaa ya ncini.

Amesema kutokana na hali hiyo hivi sasa usafiri wa anga imekuwa ni biashara na huduma inayoweza kutumiwa na watu matajiri pekee jambo ambalo linahitaji kuangaliwa zaidi ili sekta hiyo ya anga iweze kukua zaidi .

Ameshauri kwamba kutokana na mazingira ya Tanzania kunahitajika kuwepo mfumo wa kodi unaolenga hali halisi ya nchi ili uweze kusaidia nci katika kukusanya kodi na kucania ukuaji wa ucumi kama zinavyofanya nci nyenine mbali mbali.

Ameshauri pia kuwepo na mamlaka chache za kodi ili kuondosha usumbufu kwa wafanyabiashara kusimamiwa na taasisi nyingi za kodi jambo litakalochangia kukua kwa biashara ndani ya nchini.

Kwa upande wake Mwekiti wa Tume hiyo Balozi Ombene Sefue, amesema kwamba tume hiyo imepewa jukumu la kukutana na wadau mbali mbali ili kuangalia mfumo wote wa kodi na kuwasilisha serikalini mapendekezo ya kuboresha mfumo wa kodi Tanzania.

Amesema kwamba hatua hiyo ni kuisaidia serikali kufanya marekebisho na kuufanya mfumo wa kodi ulipo nchini kuwa na raisi na kuweka mazingira mazuri ya kibiasara hapa Tanzania.

Tume iyo imeundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluu Hassan na ilizinduliwa mnamo Oktoba nne mwaka huu na imepewa jukumu la kuhakikisha wanafanya mapitio kwenye mfumo wote wa kodi vikiwemo, usimamizi , mamlaka za kodi, mausinano na viwangio, umihimu wa kodi na mengineyo na kupeleka mapendekezo serikali juu ya kufanya mfumo wa kulipa kodi kuwa rahisi .

Mwisho

Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia kitengo chake cha habari leo Jumatatu Tarehe 16 Disemba 2024.


Related Posts