Serikali Yaweka Mkazo Katika Kujenga Uwezo wa Viongozi wa Mitaa kwa Ufanisi wa Miradi ya Maendeleo

Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

Imeelezwa kuwa na viongozi wa serikali za mitaa wenye ufanisi mkubwa na uadilifu mkubwa katika utendaji wa kutumia rasilimali zilizopo kuongoza jamii itasaidia nchi kuwa na ufanisi mkubwa sana katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe, Festo Dugange wakati alipomuwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mohamed Mchengerwa katika Mkutano wa wadau wa serikali za mitaa katika kuhamasiaha utawala bora ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa umma leo Jijini Dodoma.

Ndugange amesema tunaendelea kujenga uwezo kwa viongozi wa serikali za mitaa kujua majukumu yao, na kujua mipaka yao na wajibu wao wa kuwahudumia na kuwaongoza wananchi.

“Mafunzo haya yatatupa kitu cha ziada zaidi kwenda kuendelea kuwajengea uwezo viongozi wetu wa serikali za mitaa na tunaamini malalamiko na kero nyingi za wananchi ambazo ziko ndani ya uwezo wao zitatauliwa kwa ufanisi mkubwa,” alieleza Naibu Dugange.

Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuimarisha utendaji kazi serikalini na hasa katika ngazi ya serikali za mitaa ili kufikia malengo ya kitaifa katika kukuza uchumi na kuimarisha ustawi wa jamii.

Amebainisha Serikali za Mitaa, zikiongozwa na Baraza la Madiwani zitaendelea kuwa chombo huru katika kufanya maamuzi ya kisera na utendaji kwa mujibu wa sheria za nchi bila kuingiliwa na taasisi au chombo kingine.

Aidha Serikali Kuu ikiwa ni pamoja na wizara na idara za serikali yataendelea kusaidia na kuwezesha Serikali za Mitaa katika kutimiza majukumu ya msingi ya utoaji wa huduma kwa wananchi.
“Serikali za mitaa zitaendelea kuwa jukumu la kuratibu mambo ya wananchi yanayohusu maisha yao ikiwa ni pamoja na kupanga na kutekelza program za miradi ya maendeleo wa kijikita katika kukuza mahusiano ya taasisi binafsi na vikundi vya kiraia,” alisema.

Lengo la serikali ni kuona jinsi mamlaka zetu za Serikali za Mitaa zinavyojikita katika kubuni vyanzo vya vipya vya mapato na kusimamia inavyotakiwa ili kuweza kukusanya vizuri na kwa ufanisi.

“Ili wananchi waone tija ya sisi mamlaka ya Serikali za Mitaa lazima wanachi waone matunda ya usimamizi na utekelezaji wa kazi zetu za miradi ya maendeleo zinakamilika kwa wakati na kwa ubora,” alihimiza






Related Posts