Kinondoni Dar es Salaam 16 Disemba 2024 Ikiwa ni sehemu ya Kampeni yake ya kuhamasisha watanzania kutunza mazingira kwa kupanda miti 1,000,000 nchini kote, Kampuni ya Bayport leo imepanda miti 500 katika Shule ya Sekondari Mbweniteta iliyopo wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, huku Mkuu wa Wilaya hiyo, Saad Mtambule akitoa wito kwa wakazi wa wilaya ya Kinondoni kuendeleza tabia ya kupanda miti ili kukabiliana na changamoto za tabia nchi.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Bayport Tanzania, Nderingo Materu alisema kampeni hiyo ya kupanda miti waliyoanza Temeke jijini Dar es Salaam na licha ya kuhamasisha jamii ya watanzania kuona umuhimu wa kupanda miti, bali wanafanya hivyo pia kuunga mkono juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia mikakati na sera zake endelevu za uhifadi na usimamizi wa mazingira.
Alisema Kupungua kwa misitu kwa sababu ya uvunaji misitu usiokuwa endelelevu, ongezeko la shughuli za viwanda duniani, kupungua kwa theluji, mabadiliko ya utaratibu wa mvua , mafuriko, na ukame miongoni mwa jamii nyingi ulimwenguni umekuwa ukisababisha athari hasi za mabadiliko ya tabianchi.
Ili jamii yetu kujinusuru kutoka kwenye changamoto hizi zinazosabanishwa na mabadiliko ya tabia nchi tumeamua kuungana na Serikali kwa kusikiliza kusikiliza ushauri wataalam wa Mazingira kutoka NEMC kupanda miti Kwa wingi katika jamii zetu ili kuokoa maisha ya viumbe hai wengine pamoja na binadamu”
‘Bayport Financial Services Tunatoa shukurani za dhati kwa wale wote waliosaidia kwenye kampeni hii ya kupanda miti 500 hapa shule ya Sekondari ya Mbweniteta hususani Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule pamoja na Afisa Mazingira na Maliasili wa wilaya Hawa Hanti’, alisema Materu.
“Hatuwezi kuwasahau watoto na walimu wote wa shule hii, kwani wao ndio watakaohusika kwa kiasi kikubwa kuhakikisha miti hii inaendelea, sisi kama Bayport tutakuwa mstari wa mbele katika kushiriki kampeni mbalimbali za uhifadhi wa mazingira ili nchi yetu iwe mahali salama pa kuishi kutokana na uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na mabadiliko ya tabia nchini”, aliongeza Bwana Materu.
Aidha Gema John ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu Mbweniteta, alisema kuwa awali miti mingi iliyopandwa shuleni kwao ilikuwa ya kivuli lakini sasa wanaishukuru Bayport kwa kuwaletea miti ya matunda itaayowapa kivuli na lishe.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule akiongoza zoezi la upandaji miti 500 kwenye shule ya sekondari ya Mbweniteta ambayo ilitolewa na kampuni ya Bayport. Kampuni ya Bayport ipo kwenye kampeini ya kupanda miti 1,000,000 kwa lengo la kuhamasisha jamii ya watanzania kuona umuhimu wa kupanda miti na pia kuunga mkono juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia mikakati na sera zake endelevu za uhifadi na usimamizi wa mazingira.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Bayport Tanzania, Nderingo Materu akipanda moja ya miti 500 ambayo kampuni hiyo ilitoa kwa shule ya sekondari ya Mbweniteta ya wilaya ya Kinondoni. Kampuni ya Bayport ipo kwenye kampeini ya kupanda miti 1,000,000 kwa lengo la kuhamasisha jamii ya watanzania kuona umuhimu wa kupanda miti na pia kuunga mkono juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia mikakati na sera zake endelevu za uhifadi na usimamizi wa mazingira.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule akiongea na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mbweniteta mara baada ya zoezi ya upandaji miti 500 ambayo ilitolewa na kampuni ya Bayport. Kampuni ya Bayport ipo kwenye kampeini ya kupanda miti 1,000,000 kwa lengo la kuhamasisha jamii ya watanzania kuona umuhimu wa kupanda miti na pia kuunga mkono juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia mikakati na sera zake endelevu za uhifadi na usimamizi wa mazingira.