Bwana harusi aliyepotea adaiwa kupatikana Kigamboni

Moshi. Ndugu wa Vincent Masawe, bwana harusi anayedaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha wamethibitisha kupatikana kwa ndugu yao.

Kwa mujibu wa ndugu hao, Vincent amedai yupo katika kituo cha polisi kilichopo Kigamboni, mkoani Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwananchi, Vick Massawe amethibitisha kupatikana kwa ndugu yao jana asubuhi Desemba 16, 2024.

Taarifa za kupotea kwa Vincent zilifikishwa Kituo cha Polisi Kigamboni Novemba 19, 2024 na mke wake. Jeshi la Polisi katika taarifa lilisema upelelezi ulianza mara moja.

Endelea kufuatilia Mwananchi.

Related Posts