Kocha wa Simba, Fadlu Davids amesema kuwa timu yake inaingia kwa tahadhari kubwa katika mechi dhidi ya Kengold kesho katika Uwanja wa KMC Complex, Mwenge licha ya wapinzani wao kushika mkia kwenye msimamo wa ligi.
Davids amesema kuwa ugumu wa mchezo huo wa kesho unatokana na ulazima wa Kengold kuondoka na pointi tatu ili ijinasue kutoka katika nafasi mbaya iliyopo sasa.
“Wapo chini na hawana cha kupoteza hasa wanapocheza na timu kama Simba hivyo na kwa sababu ya nafasi na pointi walizonazo wana uhitaji mkubwa wa pointi.
“Kwa hiyo hatuwezi kuingia kwa kuwadharau au tukifikiria pointi tatu ni zetu. Tunatakiwa kufanya kazi kubwa,” amesema Davids.