HALMASHAURI YA MOSHI YASIMAMISHA SHERIA YA KUTOZA KODI SHEREHE.

Na WILLIUM PAUL, MOSHI.

BARAZA la Madiwani wa halmashauri ya Moshi mkoani Kilimanjaro, limesimamisha kwa muda utozwaji wa kodi katika shughuli za sherehe mpaka hapo wananchi watakapopewa elimu ya kutosha ili kuondoa malalamiko.

Kauli hiyo imetolewa leo katika kikao cha Baraza la Madiwani cha kawaida na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Morris Makoi ambapo alisema kuwa wamelazimika kusimamisha sheria ndogo hiyo namba 39 ya mwaka 2024 baada ya kusikiliza maoni ya wananchi kuwa jambo hilo ni geni kwao.

” Sheria hii ilikuwa ikitaka tozo kwenye sherehe ndogo ambapo mshereheshaji (mc) alipaswa kulipia elfu hamsini, Mpishi, mcheza mziki, mapambaji na msambazaja vinywaji kila mmoja kulipia elfu kumi” Alisema Makoi.

Alisema kuwa, kama maelekezo ambayo yamekuwa yakitolewa mara kwa mara na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha wananchi wanaridhika na huduma zinazotolewa pamoja na sheria zinazotekelezwa ziwe rafiki kwao na sio sheria kandamizi hivyo wamelazimika kusimamisha sheria hiyo kutoa fursa kwa halmashauri kutoa elimu kwa wananchi. 

Related Posts