Simba kama Yanga tu Chamazi

KAMA ilivyo kwa Mabingwa Ligi Kuu Bara, Yanga wamekuwa na bahati kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi ndivyo ilivyo kwa Simba Queens na mechi nane ilizocheza hapo imeshinda zote.

Simba hadi sasa iko nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa Ligi ya Wanawake (WPL) ikiongoza msimamo na pointi 37 baada ya mechi 13 ikishinda 12 na sare moja huku JKT Queens ambayo iko nafasi ya pili na pointi 28 ikipoteza mechi mbili.

Kwenye timu tatu zinazoongoza kwenye msimamo Simba ndio timu iliyoshinda michezo yake yote ikiwa Chamazi, mzunguko wa kwanza na mechi mbili za mzunguko wa pili.

Imepata ushindi wa mabao zaidi ya matatu huku Hat-trick zikitawala ikianza na Ceasiaa 5-0 mabao matatu ya Asha  Mnunka, Baobab 5-2, Yanga Princess 1-3, JKT 0-3,  Alliance Girls 7-0 Hat-trick ikifungwa na Jentrix Shikangwa na mzunguko wa pili ikianza kuichapa  Yanga 3-1 na JKT 2-0.

Zikiwa zimesalia mechi tano WPL kutamatika, ili kuchukua ubingwa, Simba inahitaji kushinda mechi tatu kati ya tano na itakuwa imefikisha pointi 46 ambazo haziwezi kufikiwa na JKT ambayo ikishinda mechi zote itakuwa na 43.

Kocha wa timu hiyo, Mussa Hassan ‘Mgosi’ alisema kikubwa kila mechi ni kuingia kutafuta ushindi ili wajiweke kwenye nafasi nzuri ya kuchukua ubingwa.

“Kwanza nawapongeza wachezaji wangu kwa kupambana na sisi mechi zilizosalia hatutaingia kwa kushinda mechi kadhaa tunahitaji ushindi wa pointi tatu zote zilizosalia japo haitakuwa rahisi.”

Related Posts