WAZIRI SIMBACHAWENE AZIDI KUSISITIZA UZINGATIWAJI WA MAADILI KWA WATUMISHI WA UMMA

WAZIRI  wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe.George Simbachawene,akizungumza leo Disemba 17,2024 jijini Dodoma  wakati akifungua kikao kazi cha wakuu wa idara za utawala na usimamizi wa Rasilimaliwatu katika utumishi wa Umma kilichoanza leo kwa siku tatu.

SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe.George Simbachawene (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi cha wakuu wa idara za utawala na usimamizi wa Rasilimaliwatu katika utumishi wa Umma kilichoanza leo Disemba 17,2024 jijini Dodoma kwa siku tatu.

SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe.George Simbachawene (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi cha wakuu wa idara za utawala na usimamizi wa Rasilimaliwatu katika utumishi wa Umma kilichoanza leo Disemba 17,2024 jijini Dodoma kwa siku tatu.

Naibu Waziri Ofisi wa Raisi,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bwana Deus Clement Sangu,akizungumza  wakati wa kikao kazi cha wakuu wa idara za utawala na usimamizi wa Rasilimaliwatu katika utumishi wa Umma kilichoanza leo Disemba 17,2024 jijini Dodoma kwa siku tatu.

Naibu Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais Menejimeti ya Utumishi wa umma na utawala bora na Mwenyekiti na Mratibu Mkuu wa Kikao hicho Bw.Juma Mkomi,akitoa taarifa ya kikao kazi cha wakuu wa idara za utawala na usimamizi wa Rasilimaliwatu katika utumishi wa Umma kilichoanza leo Disemba 17,2024 jijini Dodoma kwa siku tatu.

 Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Utumishi wa Umma Bi.Felister Shuli,akizungumza  wakati wa kikao kazi cha wakuu wa idara za utawala na usimamizi wa Rasilimaliwatu katika utumishi wa Umma kilichoanza leo Disemba 17,2024 jijini Dodoma kwa siku tatu.

   

WAZIRI  wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe.George Simbachawene,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua kikao kazi cha wakuu wa idara za utawala na usimamizi wa Rasilimaliwatu katika utumishi wa Umma kilichoanza leo kwa siku tatu.

Na.Alex Sonna-DODOMA

WAZIRI  wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe.George Simbachawene,amekemea tabia ya baadhi ya Maafisa Rasilimaliwatu nchini  wanaokataa watumishi wanaopangiwa majukumu katika maenee yao ya kwa mujibu wa sheria.

Mhe.Simbachawene,ametoa kauli hiyo leo Disemba 17,2024 jijini Dodoma  wakati akifungua kikao kazi cha wakuu wa idara za utawala na usimamizi wa Rasilimaliwatu katika utumishi wa Umma ambapo amesema wapo baadhi ya viongozi ambao hukataa watumishi kwa kuwa hawakutokana na wao hali inayosababisha shughuli za serikali kutofanyika kwa ufanisi.

Amesema Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeendelea kupokea malalamiko ya watumishi wanaokataliwa kupokelewa katika vituo wanavyohamishiwa au kuajiriwa.

“Siku za hivi karibuni, kuna mambo yemejitokeza ambayo sio ya kawaida na ni mapya kabisa katika utumishi wa umma.  Baadhi ya mambo hayo ni kwa Waajiri kuchagua aina ya watu wa kufanya nao kazi, kutopokea, kukataa na kuficha barua zenye maelekezo mahsusi ikiwemo barua za uhamisho (kuhamia na kuhama).”

Ameongeza kuwa “Ninyi mliopo humu ndio washauri wakuu wa Waajiri wenu.  Haya yanayofanyika ni kinyume cha utaratibu na ni utovu wa nidhamu, na hayavumiliki endapo kweli tunataka kujenga utumishi wa umma na hapa nitoe melekezo kwa utaratibu huu mpya uachwe kwa kuwa kinachofanyika ni kinyume na utaratibu.”amesisitiza Mhe.Simbachawene

Aidha amesisitiza umuhimu wa kuzingatia kwa maadili kwa Watumishi wa Umma kwani kumekuwa na malalamiko ya uvunjifu wa maadili kama vile uwepo wa Rushwa,lugha zisizofaa na udanganyifu wa nyaraka kama vile kughushi barua za masuala mbalimbali ya kiutumishi.

“Nawatka  wote wanaojihusisha  na tabia hizo kuacha mara moja na Taasisi ambazo Watumishi wake wamaebainika kuwa na mapungufu yaliyoanishwa mamlaka ya nidhamu ya watumishi katika Taasisi hizo ichukue hatua stahiki dhidi ya watumishi hao kwa majibu wa taratibu za Utumishi wa Umma. “amesema Waziri Simbachawene

Hata hivyo  ameongeza kuwa Serikali inatambua wajibu wa watumishi wa Umma unaendana na haki zao,hivyo Serikali kupitia ofisi hiyo kwa mwaka 2023/2024 imewapandisha vyeo watumishi 229,159,kuwabadilisha kada Watumishi 9,654 na kutoa nyongeza ya mshahara wa mwaka Watumishi wake na kutoa vibali vya ajira kwa kada mbalimbali.

” Serikali imetoa nyongeza ya mwaka ya mshahara kwa watumishi wake na itaendelea kuboresha maslahi ya watumishi kulingana na uwezo wa uchumi. Ni jukumu lenu kama wasimamizi wa watumishi wa Umma kuendelea kuwasimamia watumishi walio chini yenu kwa kuwaelimisha kuhusu haki na wajibu wao ili wanapodai haki wajue kuwa kuna wajibu wanapaswa kuwa wametekeleza”amesema 

 Amesema kuwa  Katika mwaka wa Fedha 2024/2025 Serikali imetoa kibali cha kuajiri watumishi arobaini na tano elfu na themanini (45,080) wa kada mbalimbali, kati yake watumishi elfu kumi mia tatu tisini na sita (10,396) ni wa Kada za Afya, watumishi elfu kumi mia tano tisini (10,590) wa kada za Ualimu na Watumishi elfu ishirini na nne na tisini na nne (24,094) wa Kada nyingine.

“Nimetaarifa kuwa mchakato wa ajira wa watumishi wa kada za Afya umekamilishwa na watumishi hao tayari wameshapangiwa vituo vya kazi. Niwatake waajiri kuhakikisha wanawapatia mafunzo ya awali, kuwalipa stahiki zao na wanawajengea uwezo.  Vilevile, ni wajibu wa Waajiri wote kutenga bajeti kwa ajili ya Ajira mpya kulingana na mahitaji halisi ya Taasisi zao”.amesema

Pia Katika kutekeleza dhana ya uwazi na uwajibikaji Ofisi ninayoiongoza imeweka Mifumo ya uwazi na uwajibikaji kupitia “Sema na waziri utumishi” na e-Mrejesho ili kupokea mrejesho wa watumishi na wananchi kwa ujumla.

Aidha, kwa sasa Ofisi inaendelea na usanifu wa Daftari la Kielekroniki la Huduma za Serikali (Government Service Directory) ambalo baada ya kukamilika kwake itawezesha wananchi na watumishi kufahamu huduma zinazotolewa na Taasisi za Umma, gharama kama zipo na michakato ya kufuatwa katika kupata huduma hizo. Uwepo wa Daftari hilo utasaidia kudhibiti Vishoka wanaoingilia huduma zinazotolewa na Serikali kwa sababu huduma zote zinazotolewa na Serikali zitakuwa wazi.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi wa Raisi,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bwana Deus Clement Sangu amesema kuwa kikao hicho kinatoa fursa ya kuweka msisitizo wa uzingatiaji wa Sheria,Kanuni,Taratibu na Miongozo katika usimamizi wa Rasiliamali watu katika Utumishi wa Umma. 

Awali akitoa taarifa ya Kikao hicho Naibu Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais Menejimeti ya Utumishi wa umma na utawala bora na Mwenyekiti na Mratibu Mkuu wa Kikao hicho Bw.Juma Mkomi,amesema kuwa kayika kikao hicho cha siku tatu mada mbalimbali zijadiliwa pamoja na kukumbushana umuhimu wa utumishi wa umma..

“Mheshimiwa Mgeni, kikao hiki kinatoa fursa ya  kutoa maelekezo muhimu kwa washiriki kuhusu masuala mbalimbali ya utawala na usimamizi wa Rasiliamali watu katika Utumishi wa Umma, kuweka maazimio mbalimbali ya kiutendaji kwa lengo la kuboresha zaidi utawala na usimamizi wa Rasiliamali watu katika Utumishi wa Umma, kueleimisha juu ya masuala mtambuka yanayohusu Afya ya Akili,fursa za uwekezaji kwa watumishi wa umma na umuhimu wa maadili katika kuweka mazingira bora ya usimamiz wa Rasilimaliwatu katika utumishi wa umma “.amesema Bw.Mkomi

Related Posts