Singasinga wakabidhi msaada Makao ya Watoto New Life

JAMII ya Singasinga Mkoa wa Dar es Salaam, leo Desemba 17,2024 imekabidhi sadaka ya bidhaa mbalimbali katika Makao ya Kulea Watoto ya New Life, Tegeta, wilayani, Kinondoni , mkoani Dar es Salaam na kuahidi kuendelea kushirikiana na jamii katika malezi ya watoto na kusaidia watu wenye mahitaji maalumu.

Akikabidhi sadaka hiyo, Mwakilishi wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Dar es Salaam, Inderpreet Kaur Saini,alisema ni katika kuadhimisha kitendo cha watoto wanne wa Mtume wa 10 wa Singasinga, Guru Gobind Singh, kutolewa maisha yao kwa kutete msimamo wa imani yao miaka 320 iliyopita.

Alisema, katika kukumbuka matendo mema ya watoto hao na maelekezo ya dini yao, Singasinga Mkoa wa Dar es Salaam, wanajihusisha na matendo ya huruma katika jamii ikiwa ni pamoja na kusaidia watoto wanaolelewa katika vituo maalumu.

“Sisi hatuwaiti hawa watoto yatima. Tunawaona ni watoto wa kawaida kama wanaolelewa na familia zao kwa sababu sote tuna wajibu wa kuwalea. Ndiyo maana tumekuja kuwapatia mahitaji mbalimbali tukitambua wajibu wetu wa kuwalea,”alisema Inderpreet.Alitaja msaada uliokabidhiwa kuwa ni pamoja na vifaa vya shule, chakula, vinywaji, vifaa vya usafi, vifaa vya michezo na tauro za kike.

Inderpreet, alisema katika matukio hayo, Singasinga wamekuwa wakiwashirikisha vijana waoa kuhudumia watoto wenzao wenye mahitaji maalumu lengo likiwa kuwa jengea tabia ya kushirikiana,kutoa, kusaidia na kukua katika misingi ya kuamini Mungu ni mmoja.

“Watoto wa kiume wanne wa Guru Gobind Singh Ji ni Baba Ajit Singh Ji, Baba Jujhar Singh Ji Baba Zorawar Singh Jin a Baba Fateh Singh Ji, ambao walitolewa maisha yao wakiwa wanapigana dhidi ya dhuruma wakiwa katika umri mdogo wa miaka tisa, saba, 14 na 16,”alieleza.

Alisema,imami ya Singasinga, inasimamia nguzo kuu tatu ambazo ni kufanya swala, kufanya kazi yoyote halali na nguzo ya tatu ni kusaidia jamii hasa wasiyo kuwa nacho.

Alisema, jamii hiyo inataendelea kuheshimu misingi ya dini hiyo na dini zingine na kutoa misaada yake bila kujali tofauti za kidini kwani wanaimani kila dini ina mwelekea Mungu mmoja tu.

“Sisi hatujali tofauti za dini. Binadamu wote ni sawa na ni wa Mungu mmoja, hivyo tutashirikiana na jamii nzima,”alisema. Katika hafla hiyo, Singasingaia walikula chakula cha mchana na watoto wa kituo hicho.

Akipokea msaada huo, Katibu wa kituo hicho Mbwana Kondo, alisema kituo hicho kina lea watoto 93 wenye umri na jinsia tofauti ambapo wenye umri mdogo kabisa ni mapacha wa miezi nane.Kondo alieleza, msaada huo ni muhimu kwani unagusa mahitaji ya msingi ya elimu, chakula, michezo na afya hivyo kuishukuru jamii ya Singasinga.


 

Related Posts