Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano kutoka Airtel, Jackson Mmbando na Meneja Huduma kwa Wateja kutoka Airtel, Celine Njuju wakionesha moja ya zawadi ambazo zitatolewa katika msimu huu wa sikukuu.
Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano kutoka Airtel, Jackson Mmbando akizungumza jijini Dar Es Salaam leo Desemba 17, 2024, ikiwa ni katika kusheherekea sikukuu ya Christimas ambapo watatoa zawadi mbalimbali kwa wateja wao.
Meneja Huduma kwa Wateja kutoka Airtel, Celine Njuju akizungumza jijini Dar Es Salaam leo Desemba 17, 2024, ikiwa ni katika kusheherekea sikukuu ya Christimas ambapo watatoa zawadi mbalimbali kwa wateja wao.
KAMPUNI ya Airtel Tanzania imezindua promosheni ya Airtel Santa Mizawadi nchini Kwa kuwazawadia wateja na mawakala.
Akizungumza jijini Dar Es Salaam leo Desemba 17, 2024, ikiwa ni katika kusheherekea sikukuu ya Christimas, Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano, Jackson Mmbando amesema Airtel Tanzania inaanza msimu huu wa sikukuu na Airtel Santa Mizawadi ambayo ni promosheni maalum yakutoa shukrani na kuwazadia wateja na mawakala wote wanaoendelea kutumia huduma za Airtel katika msimu wa sikukuu.
Airtel Santa Mizawadi ni ipo kabambe na itawapatia washindi fursa ya kuondoka na zawadi kemkem ikiwemo pocket WiFi, simu janja, pikipiki, runinga na pesa Taslim hadi shilingi milioni moja.
“Jinsi ya kushirikina kujishindia Mizawadi ya Airtel Santa Mizawadi, ikiwa awewe ni Wakala wa Airtel unatakiwa tu kufanya miamala ya kuweka na kutoa fedha, ambapo pia ili Mteja aweze kuingia kwenye droo anatakiwa tu kufanya miamala kama vile kununua bando, Kutuma pesa, kutoa pesa, kulipa bili, kufanya miamala ya kibenki, kutuma au kupokea pesa nje ya nchi, kununua muda wa maongezi au vifurushi kupitia *149*99#, *150*60#, au kwa kutumia ‘My Airtel App’.”
Mmbando, ameeleza kuwa Promosheni ya Airtel Santa Mizawadi ni inalenga kuwashukuru wateja na mawakala waaminifu na wanaoendelea kutumia Airtel katika msimu wote huu wa sikukuu.
“Kupitia Promosheni ya Airtel Santa Mizawadi tunasambaza upendo na kunogesha sikukuu kwa wateja na mawakala wetu wetu ambao wamekuwa na mchango mkubwa katika mafanikio yetu,” amesema Mmbando.
Amesisitiza kuwa Airtel inaendelea kujidhatiti kutoa huduma za kipekee katika msimu wa sikukuu huku akidokeza kuwa kila muamala unaofanyika unatoa nafasi kwa wateja au mawakala kujishindia zawadi zitakazoboresha Maisha.
Kwa upande wake Meneja Huduma kwa Wateja, Celine Njuju amesema … “Airtel tunawadhamini sana wateja wetu, Tusingefika hapa tulipo leo bila ya wateja na mawakala wetu, Airtel Santa Mizawadi ni promosheni kabambe kwa kuwa itanogesha balozi wetu, mtamuona Mr SANTA wetu akitembelea baadhi ya mitaa yetu kuhakikisha wateja na mawakala wanapata pia zawadi za papo kwa hapo, ikiwa utabahatika kukutana nae basi nakuahidi atanogesha msimu wako wa sikukuu vizuri ufurahie wewe na wapendwa wako.”
Amesisitiza kuwa washindi wa Airtel Santa Mizawadi watapatikana kupitia Droo za zitakazochezwa kila wiki mara moja ambapo washindi wote watapigiwa simu kupitia namba maalum ya Airtel 100.