Wananchi wasisitizwa kutunza vyanzo vya maji

Bodi ya maji Bonde la Wami Ruvu imeendelea kusisitiza wananchi kuacha kufanya shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo vya maji kwa kuzingatia Sheria za mita sitini

Wito huo umetolewa na mwanasheria bodi ya maji Bonde la Wami Ruvu Aloyce Lyimo wakati akizungumza jukwa la wadau wa maji wa kidakio cha Wami ambapo amesema licha ya elimu kutolewa bado kumekua ya uharibifu na uvamizi wa vyanzo vya maji.

Amesema suala la kutunza vyanzo vya maji ni jukumu la kila la mtu sio la Bode la Wami peke yake hivyo watendaji wa vijiji na wenyeviti wanatakiwa kutoa elimu kwa wananchi.

Akizungumza katika jukwa Hilo kaimu ya Maji Wami Ruvu Mhandisi Amy Mchele amesema kuwa ina imani kubwa na Jukwaa la Wadau Kidakio Cha Wami litakuwa na uwezo wa kupambana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika kidakio hicho


Mhandisi Amy amesema kuwa wadau hao wanajukumu la Kuandaa mikakati thabiti katika kulinda rasilimali za maji ikiwemo usimamizi wa sheria,utekelezaji wake pamoja na kutoa elimu hasa Kilimo ,uvuvi na ujenzi Katika maeneo hayo.

 

Related Posts