Dirisha dogo la usajili tayari limekwisha kufunguliwa tangu Desemba 15, klabu mbalimbali zimeanza kufanya maboresho ya timu zao ili kuongeza nguvu na kufanya vizuri nmzunguko wa pili wa Ligi.
Katika kufanya maboresho wapo watakaopunguzwa na wengine kuongozwa.
Ikiwa inauelekea mchezo mgumu wa Ligi Kuu Bara leo dhidi ya Simba utakaochezwa kwenye Uwanja wa KMC Complex kuanzia saa 10:00 Jioni, Ken Gold imetangaza kuachana na n yota wake watano.
Hadi sasa KenGold imecheza mechi 14 ikishika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 6. Imeshinda mechi 1, Sare 3 na kupoteza mechi 10.