Tanzania na Shirikisho la Jamhuri ya Somalia zinatarajia kufanya mazungumzo yanayolenga kuibua maeneo mapya ya ushirikiano na kuongeza uhusiano wa kidiplomasia na uchumi yatakayofanyika jijini Mogadishu kuanzia tarehe 17 -19 Disemba 2024.
Ujumbe wa Tanzania tayari umeanza kuwasili nchini humo kushiriki katika vikao vya ngazi ya Wataalamu ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mkutano wa ngazi ya Mawaziri unaotarijiwa kufanyika tarehe 19 Disemba 2024.
Katika mazungumzo hayo Tanzania itawakilishwa na ujumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Wizara ya Utalii, Wizara ya Afya na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.