Serikali kuongeza ulizi Kwa Mkapa, kamera 200 kufungwa

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amewaonya mashabiki wa mpira wa miguu wanaofanya vurugu uwanjani akisema watashughulikiwa, kwani Serikali ina ukarabati kwa kuweka kamera zaidi ya 200.

Kauli hiyo ameitoa leo Desemba 18, 2024 katika mkutano wa Waziri Wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na wadau wa habari.

“Ukarabati unaofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa ni mkubwa. Tunafunga camera zaidi ya 200, ukivunja kiti tuta deal na wewe,” amesema

Desemba 15 zilitokea vurugu wakati wa mechi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baina ya Simba dhidi ya CS Sfaxien katika huo na kusababisha uharibifu wa viti zaidi ya 200 pamoja na kujeruhi baadhi ya mashabiki.

Awali akitoa salamu kwa Waziri, Mwenyekiti mstaafu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (Taswa), Abdallah Majura alimshauri Serikali kuwaadhibiti mashabiki wanaofanya vurugu kwa kuwazuia kuingia uwanjani.

Related Posts