Ukraine wakiri kufanya mauaji ya Jenerali wa Urusi na msaidizi wake mjini Moscow

 

IDARA ya usalama ya Urusi imesema, kijana mwenye umri wa miaka 29 kutoka Uzbekistan amekamatwa akituhumiwa kwa mauaji ya Luteni Jenerali Igor Kirillov na msaidizi wake huko Moscow. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Mkuu wa Kikosi cha Ulinzi cha Nyuklia, Biolojia na Kemikali, aliuawa Jumanne wiki hii, nje ya makazi yake baada ya kilipuzi kilichofichwa kwenye skuta kumlipukia.

Mshukiwa anadaiwa kusajiliwa na shirika la ujasusi la Ukraine; mauaji hayo yalipangwa na idara ya usalama ya taifa hilo lilivovamiwa na Urusi.

Luteni Jenerali Igor Kirillov (54), aliyekuwa mkuu wa silaha za kemikali wa Urusi, “alilengwa kimaksudi” kwa kuwa alitekeleza uhalifu wa kivita nchini Ukraine.

Siku moja kabla ya mauaji yake, Ukraine ilimshtaki Kirillov, bila kuwapo mahakamani, ikisema “alihusika na matumizi makubwa ya silaha za kemikali zilizopigwa marufuku.”

Mkuu wa vikosi vya nyuklia, biolojia na kemikali (NBC), alikuwa kwenye mlango wa kuingia kwenye makazi ya watu mapema Jumanne, wakati kifaa kilichofichwa kwenye pikipiki kilipolipuka na kumuua.

Kifaa hicho kiliripuka kwa mbali na kilikuwa na milipuko yenye uzito wa gramu 300, vyanzo vya usalama vya Urusi vimeliambia shirika la habari la serikali la Tass.

Wakati Luteni Jenerali Igor Kirillov na msaidizi wake Ilya Polikarpov walipouawa kwa bomu, ukweli wa vita vya Urusi dhidi ya Ukraine ulionekana dhahiri mbele ya macho yao kwa raia wake.

About The Author

Related Posts